Kiswahili

Tafakari 21: Unapendwa.  Amini hilo.

Kukubaliwa na Kristo na kuishi ndani ya Moyo Wake wenye huruma kutakuwezesha kugundua jinsi anavyokupenda sana.  Kwa kweli anakupenda zaidi ya unavyoweza kuwazia.  Jiruhusu kuanza kuugundua upendo huo.  Uonje, uuamini, uuelewe na utafute zaidi na zaidi…

Soma zaidi

Tafakari ya 20: Mkabidhi Yesu Maisha Yako Kila Siku

Yesu akishakupokea na kuifanya roho yako kuwa mali Yake, usiwe na wasiwasi kuhusu kitakachofuata. Usitarajie maisha yabadilike sana mara moja, lakini pia usishangae yakibadilika hivyo. Jambo pekee la maana ni kwamba kila siku unafanya upya kujitoa kwako Kwake…

Soma zaidi

Tafakari ya 19: Bwana Anakukubali katika Huruma Yake

Ikiwa kwa kweli umemtafuta Bwana wetu aliye Mungu, basi mwulize kama atakukubali ndani ya Moyo Wake na katika Mapenzi Yake matakatifu.  Mwulize na umsikilize.  Ikiwa umekabidhi yote na kujitoa Kwake, atakujibu akikuambia kwamba anakukubali.  Mara tu…

Soma zaidi

Tafakari ya 18: Huruma Inayotolewa Kupitia Mapadri

Huruma hutolewa kwa njia nyingi. Kati ya njia nyingi za Huruma, itafute kupitia mapadri watakatifu wa Mungu. Mruhusu padri Wake akusikilize, azungumze nawe na akuongoze. Mapadri ni dhaifu na ni wenye dhambi. Lakini katika udhaifu wao wanapewa neema ya pekee ya kuongoza roho. …

Soma zaidi

Tafakari ya 17: Mgeukie Mama Yetu Mbarikiwa kwa Sala

Mgeukie Mama yetu Mbarikiwa kwa sala yenye matumaini thabiti.  Anakukumbatia karibu na Moyo wake Safi Kabisa na atakuongoza kwa Mwanawe, Yesu.  Yeye ni Mama mkamilifu, Mama wa Neema Zote.  Tumainia uangalizi wake wa kimama na maombezi yake.  Anajua jinsi ya kufanya neema zipatikane…

Soma zaidi

Tafakari ya 16: Kujikabidhi Kabisa kwa Mungu

Sujudu mbele za Mungu. Jilaze kifudifudi mbele Yake. Ukiweza, fanya hivyo kwa mwili. Ikiwa kufanya hivyo kutawavuruga wengine, basi fanya hivyo moyoni. Jilaze kifudifudi mbele za Mungu na umsihi akuonyeshe Huruma Yake ya Kimungu na Mapenzi Yake matakatifu kabisa. Kuna nyakati nyingi…

Soma zaidi

Tafakari ya 15: Mungu Hachoki Katika Upendo Wake

Je, unaahirisha kumwitikia Mungu? Je, unapuuza wito Wake wa daima? Je, unaruhusu mambo mengi yanayokukengeusha kuizima sauti Yake? Jua kwamba Mungu haachi kamwe kukuita. Msikilize. Wakati mwingine tunaahirisha kumwitikia Mungu kwa sababu tumeamua, kimakosa, kwamba tutapata uradhi maishani kwa njia nyingine…

Soma zaidi

Tafakari ya 14: Kuridhika kwa Kweli Kupitia Huruma Pekee

Mara nyingi sana maishani tunatafuta kuridhika katika vitu vya dunia vinavyopita. Iwe ni utajiri, anasa za mwili, hadhi, au kitu kingine chochote, lazima tufikie kutambua kwamba kitu kimoja tu ndicho kinachotutosheleza. Huruma ya Mungu ndiyo tunayoitafuta. Kila kitu kingine ni udanganyifu…

Soma zaidi

Tafakari ya 13: Mwaliko Katika Ukimya

Ndani ya nafsi zetu tunapaswa kujitahidi kumsikia Mungu akisema nasi. Husema katika ukimya na katika vilindi vya nafsi. Kwanza, anatualika. Anatualika tumjue na tukutane na Huruma ya Mungu inayotiririka kutoka Moyoni Mwake. Mwaliko huo ni mwaliko tu. Yesu…

Soma zaidi