Kiswahili

Tafakari 329: Kuungama kwa Furaha

Kwa nini unaogopa kuungama?  Sakramenti hii tukufu unatolewa kutoka katika Moyo wenye huruma wa Bwana wetu.  Kwa njia ya zawadi hii tukufu, Yesu anakuondolea mizigo unayobeba ili uweze kushiriki kikamilifu zaidi katika Huruma Yake.  Kama ungeelewa hili…

Tafakari ya 322: Kizuizi cha Kiburi

Bwana, katika Huruma Yake tele, hukujia mchana na usiku na huingia katika nafsi yako kwa furaha inapokuwa wazi Kwake.  Hata mapambano makubwa zaidi hayamzuii Bwana wetu kukujia.  Lakini kuna jambo moja hasa linalomweka Bwana wetu mbali.  Nalo ni kiburi.  Kiburi ni mama wa dhambi zote…

Tafakari 318: Kutojali na Kusahau

Kama ungekuwa katika ndoa na mara kwa mara ukawa humjali mwenzi wako, hilo lingekuwa tatizo.  Kutojali maana yake ni kutokuwa na moyo wa kujali kwa dhati mema ya mwingine.  Kusahau ni dalili ya kutojali kwa kuwa mtu asipojali sana, ni rahisi kwake kusahau.  Kwa mfano…

Tafakari ya 317: Kuwahukumu Wengine

Ni rahisi sana kumhukumu mwingine, lakini ni vigumu sana kujizuia kufanya hivyo.  Kwa nini hali iko hivyo?  Kwa nini unaweza kujikuta ukiwahukumu wengine kwa urahisi ilhali kwa kweli hujui yaliyo mioyoni mwao?  Hakika kunaweza kuwa na sababu nyingi za dhambi hii; mojawapo…

Tafakari ya 316: Mwali wa Upendo Unaowaka

Kuna taswira nyingi tunazotumia kuelezea Upendo wa Mungu.  Mojawapo ni “Mwali wa Upendo Unaowaka.”  Taswira hii inaonekana katika kitabu mashuhuri cha kiroho, “Mwali Hai wa Upendo,” kilichoandikwa na Mtakatifu Yohane wa Msalaba…

Tafakari 314: Huruma kama Ulinzi Imara

Jeshi linapozingirwa, hutafuta mahali ambapo linaweza kujilinda.  Mara moja hutafuta eneo lililoinuka au mahali panapolipa hifadhi na ulinzi.  Ndivyo inavyopaswa kuwa katika maisha yako ya kiroho.  Unapopigwa na mishale ya yule mwovu, au maisha yanapokuwa…

Tafakari 311: Ukweli wa Unyenyekevu

Fadhila tukufu ya unyenyekevu inapaswa kueleweka, kutafakariwa daima na kukumbatiwa daima.  Unyenyekevu ni nini?  Si kingine ila kuujua ukweli kuhusu wewe mwenyewe, kuuamini ukweli huo na kuishi kulingana nao.  Ni wewe na Mungu tu mnaojua undani wa dhamiri yako.  Wanadamu…

Tafakari 306: Mungu Hachoki

Je, unautilia shaka Upendo wa Mungu?  Ukweli ni kwamba Mungu hachoki kukutafuta.  Ingawa sehemu kubwa ya utakatifu wetu inatutegemea sisi, sehemu kubwa zaidi inamtegemea Mungu.  Tukiwa hapa duniani, Mungu haachi kamwe kututafuta na kutaka tuongoke.  Anakutumia Huruma Yake ili…

Tafakari 300: Kufunua Siri za Nafsi Yako

Kwa kweli, inafariji sana kuwa na mtu unayeweza kumfunulia yaliyo ndani kabisa ya nafsi yako.  Mtu wa namna hii unayemwamini ni baraka kubwa anapokuhakikishia utunzaji kamili wa siri, huruma na uelewa.  Kuzungumza hata kuhusu dhambi zako bila kusita…

Tafakari 298: Virusi vya Masengenyo Yasiyo na Maana

Mwelekeo mmoja wa kusikitisha katika asili yetu ya kibinadamu iliyoanguka ni “kumsengenya” mwingine.  Ni kama virusi kwa kuwa mtu mmoja anapoanza, huenea upesi kwa wengine.  Muda si muda, watu wengi wanaweza kuwa wanaeneza uvumi na masengenyo yasiyo na msingi katika ukweli, au ukweli unaosemwa bila upendo.  Hili…