Kiswahili

Tafakari ya 169: Utulivu Mbele ya Mfalme

Kukutana na mtu mwenye mamlaka makubwa kunaweza kuleta msisimko.  Kwa mfano, kukutana na rais wa kampuni unayotamani kufanya kazi ndani yake, au kukutana na mtu maarufu kwa mara ya kwanza, au kukutana na askofu au Baba Mtakatifu, yote hayo yanaweza kuleta msisimko fulani.  Lakini…

Tafakari 168: Kuomba Huruma ya Mungu kwa Ajili ya Wengine

Kuna jambo moja, na moja tu, lenye uwezo wa kuwaokoa wenye dhambi kutoka katika moto wa jehanamu.  Jambo hilo ni Huruma.  Mungu hutoa Huruma Yake bure na kwa wingi, lakini pia amechagua kutoa Huruma Yake akiitikia sala zetu tunaposali kwa…

Tafakari ya 167: Kumtamani Bwana kwa Kiwango cha Juu Kabisa

Unaposali, na unaposali kwa muda mrefu na kwa bidii, Bwana ataingia ndani yako.  Atakuwa katika ushirika nawe na kuuunganisha Moyo Wake na wako.  Utayaona matokeo haya kwa namna mbalimbali.  Mojawapo ya matokeo ya kawaida ni kwamba kadiri unavyovutwa zaidi katika muungano na Kristo, ndivyo…

Tafakari 164: Kuwa na Shauku kwa Nafsi za Wenye Dhambi

Unapomwona mtu ambaye dhambi yake iko wazi, unaitikiaje?  Watu wengi huitikia kwa dharau na hukumu kali.  Mtu anapovunja sheria, tunamhukumu vikali.  Mtu anapoishi maisha yasiyo ya maadili, tunamdharau.  Mara nyingi sana, mtazamo wetu…

Tafakari 160: Huruma katika Kitubio

Je, umegundua furaha kubwa ya kwenda kuungama? Baadhi ya watu hawaioni Sakramenti ya Kitubio kuwa chanzo cha furaha kubwa. Badala yake, wanaiona kuwa jambo lenye maumivu na linalowaaibisha. Lakini huenda wengine wanahitaji aibu inayotokana na kuungama kwa unyofu…

Tafakari ya 159: Huruma katika Saa ya Kifo Chako

Kila tunaposali sala ya “Salamu Maria”, tunasali kwa ajili ya saa takatifu ya kifo chetu.  Kwa kufanya hivyo, tunaikabidhi saa hiyo kwa Mama yetu Mbarikiwa ili atuombee wakati tunapohitaji zaidi maombezi yake.  Sala nyingine takatifu ya kusali kwa kujiandaa kwa saa hiyo ni Rozari ya Huruma ya Mungu.  Mara nyingi mno…

Tafakari ya 157: Kufanya Maamuzi ya Kimaadili

Je, wakati mwingine unapata shida kufanya uamuzi ulio sahihi kimaadili? Hali hii hutokana na asili yetu ya kibinadamu iliyoanguka dhambini. Tunachanganyikiwa kwa urahisi maishani na tunaweza kushindwa kwa urahisi kufahamu Mawazo na Mapenzi ya Mungu. Basi ufanye nini? Jua kwamba dhamiri yako ni patakatifu ambapo…

Tafakari 156: Bwana Ndiye Kimbilio Letu

Kuna nyakati maishani ambapo hofu inakuingia.  Huenda una jukumu gumu linalokukabili, au unatembea katika njia usiyoijua.  Hali hizi, pamoja na mambo mengine mengi tunayopitia maishani, zinaweza kusababisha hofu na mahangaiko.  Hofu ya mambo usiyoyajua inaweza…

Tafakari ya 154: Kuabudu kwa Ukimya na Unyenyekevu

Wazia Mama yetu Mbarikiwa katika hali duni wakati wa Kuzaliwa kwa Yesu.  Wakati huo hakuwa na makao mengine isipokuwa mahali hapa walipokusanyika wanyama.  Hata hivyo, katika utulivu wa usiku ule mtakatifu, alijisikia kuwa nyumbani alipomtazama Mtoto wake kwa ibada ya kuabudu na upendo wa kina kabisa.  Yeye…

Tafakari 148: Huruma kwa Walio Toharani

Mpendwa wetu anapofariki, ni rahisi kudhani mara moja kwamba yuko Mbinguni na hahitaji tena sala zetu.  Lakini mojawapo ya zawadi kuu zaidi tunazoweza kuwapa waliotangulia mbele yetu ni sala zetu.  Ni kweli kwamba kila mtu anayekufa katika hali ya neema…