Kiswahili

Tafakari 269: Kutazama Mambo Mawili: Huruma na Unyonge

Kama ungeweza kuchagua mambo mawili ya kuyatazama kwa tafakari, yangekuwa yapi?  Kwa hakika, mambo mawili muhimu zaidi ya kuyatazama ni Huruma ya Mungu na unyonge wako mwenyewe.  Yaelekea unaelewa mara moja kwamba Huruma ya Mungu ingekuwa mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuyatazama…

Tafakari 268: Kutafakari Kifo

Labda kufikiria kifo chako kunakutia hofu.  Huenda si jambo unalolitafakari mara nyingi sana.  Lakini ni neema kuweza kukitazama kifo chako bila kukikwepa na kwa matumaini kamili.  Na unaweza kufanya hivyo kwa matumaini kamili ikiwa tu maisha yako yako katika hali njema…

Tafakari 267: Haki au Huruma?

Inafaa kuzungumza kuhusu Haki ya Mungu na pia Huruma Yake.  Havipingani.  Haki Yake itatekelezwa kwa wale wanaokataa kutubu, kama ilivyotekelezwa kwa malaika waliokataa kumtumikia Mungu.  Lakini, kwa sasa, inafaa zaidi kusema kwamba Mungu ni Mwenye Huruma.  Kwa kweli…

Tafakari 266: Kuvunjika Moyo Mbele ya Utakatifu

Je, unataka kuwa mtakatifu? Tunatumaini jibu ni “Ndiyo.” Lakini vipi kuhusu swali hili: Je, unafikiri unaweza kuwa mtakatifu? Huenda ikawa vigumu zaidi kujibu swali hili. Ni rahisi kuota kuhusu utakatifu na kutamani…

Tafakari 265: Hatari na Baraka ya Mihemko

Mungu alituumba tukiwa na mihemko.  Mihemko hii inaweza kuwa baraka kubwa katika safari yetu ya Kikristo, au inaweza kuwa mitego mikubwa.  Yote hutegemea kile kinachotawala kila mhemko.  Kwa mfano, mihemko ya hasira inaweza kutumiwa kwa wema au kwa uovu.  Hasira inapotutawala na chanzo cha hasira hiyo…

Tafakari ya 264: Mafungo Pamoja na Yesu

Je, umewahi kufanya mafungo?  Baadhi ya watu wana fursa ya kujitenga na pilikapilika za maisha ili kutumia muda mrefu wakimsikiliza Bwana wetu na kukaa katika uwepo Wake wenye huruma.  Wengine huona vigumu kupata hata siku moja ya kufanya mafungo kama hayo.  Hata hivyo…

Tafakari ya 263: Mungu kama Nahodha Wako katika Dhoruba

Jiwazie ukiwa mtoto mdogo katika mashua ndogo katikati ya bahari. Dhoruba inaanza, wala huwezi kuona nchi kavu upande wowote. Mawimbi yanakurusha na kukugeuza, yakifunika omo la mashua kila yanapoipiga, nawe unajiuliza utawezaje kupona. Sasa jiwazie kwamba baba yako…

Tafakari 262: Utawala wa Upendo au wa Haki

Hatuwezi kuukwepa Mkono wa Mungu.  Yeye ndiye anayeutegemeza ulimwengu na kuvidumisha vitu vyote katika uwepo.  Bila utunzaji Wake wa daima tungekoma kuwapo.  Lakini tunabaki chini ya Mkono Wake wa maongozi kwa mojawapo ya njia mbili.  Ama tunaongozwa na “utawala wa upendo” au na “utawala wa haki.”  Utawala…

Tafakari 261: Yesu Aliyejificha Ndani ya Wengine

Fikiria kama Yesu angekujia akiwa maskini, mwenye njaa na baridi, na kukuomba umtunze.  Hali hii huenda ikakushtua na kukufanya ujiulize kama kweli mtu huyo ni Yesu.  Lakini ni Yesu.  Yesu hutujia kila siku katika mtu mwenye uhitaji.  Huenda…

Tafakari 260: Ukuu wa Matendo Madogo ya Upendo

Je, unataka kufanya mambo ya kushangaza katika ulimwengu huu?  Je, wakati mwingine una mawazo na ndoto kubwa sana?  Wakati mwingine ndoto zetu huwa za kidunia zaidi, za kupata utajiri na umaarufu, na wakati mwingine tunaweza kuwa na ndoto za kufanya mambo yasiyo ya kawaida kwa ajili ya Mungu na Kanisa.  Lakini si lazima haya yabaki kuwa ndoto…