Kiswahili

Tafakari ya 13: Mwaliko Katika Ukimya

Ndani ya nafsi zetu tunapaswa kujitahidi kumsikia Mungu akisema nasi. Husema katika ukimya na katika vilindi vya nafsi. Kwanza, anatualika. Anatualika tumjue na tukutane na Huruma ya Mungu inayotiririka kutoka Moyoni Mwake. Mwaliko huo ni mwaliko tu. Yesu…

Tafakari 361: Sadaka na Sala

Ingawa huenda ikawa vigumu kuelewa na kuamini jambo hili, sadaka ya ndani iliyounganishwa na sala safi huleta manufaa makubwa ajabu kwa utangazaji wa Injili ulimwenguni kote.  Kwa kweli, kama wamisionari wasingekuwa na nguvu za watu watakatifu waliotoa kila siku sadaka za ndani…

Tafakari 348: Mungu Hutimiza Anayoyafunua

Inashangaza kuyatafakari mambo mawili ya hakika kwa pamoja.  Kwanza, tafakari jinsi Mtakatifu Faustina alivyomsikia Yesu akimwambia mara kwa mara kwamba alitaka Sikukuu ya Huruma ya Mungu itangazwe rasmi na kuadhimishwa katika Jumapili ya Pili ya Pasaka kila mwaka.  Je, mtawa huyu wa kike, mnyenyekevu aliyeishi maisha ya kujitenga monasterini, angewezaje kutimiza jukumu kama hilo…

Tafakari 338: Kutunza Siri

Tendo moja la upendo tunaloweza kumtendea mwingine ni kumtunzia siri.  Sote tumewahi kufikiwa na watu wenye tatizo au waliochanganyikiwa, nao wakatuomba tusimwambie mtu mwingine.  Je, unaweza kuitunza siri takatifu ya namna hii?  Kutunza siri ni tendo zuri sana la huruma kwa wengine.  Ikiwa…