Kiswahili

Tafakari ya 33: Huruma ya Utakaso

“Magdalena Mwenye Toba” iliyochorwa na Guido Reni

Video

Sikiliza kwa Kiingereza

Hebu fikiria kama ungeweza kuiona roho yako kama Mungu anavyoiona.  Ungeona nini?  Mungu anaionaje roho yako?  Hakika anamwona mtoto Wake wa thamani na anakutazama kwa upendo mkuu kabisa.  Lakini pia anaiona dhambi yako, hata iliyo ndogo kabisa.  Dhambi hizi, hata kasoro ndogo kabisa, lazima ziondolewe ndani yako kwa upendo Wake uwakao.  Huruma ya Mungu huwa “yenye kuumiza” sana kiroho inapotakasa.  Lakini utakaso huu ni wa lazima na huleta uhuru.  Utakaso lazima ufanyike ama sasa ama kwa kupitia toharani.  Chagua utakaso wa upendo wenye huruma wa Mungu sasa, nawe hutajuta (Tazama Shajara #36).

Tafakari leo juu ya upendo wa Mungu unaokujia ili kuitakasa roho yako kutokana na kila dhambi, hata kasoro ndogo kabisa unayoweza kuwa nayo.  Ona hili kuwa tendo la Huruma tele.  Uwe tayari kuhisi uchungu mtamu wa kutakaswa, wala usiukimbie.  Kutakaswa kwako kunaujaza Moyo wa Bwana wetu furaha kuu!

Bwana, nisaidie kuiona roho yangu kama Wewe unavyoiona.  Nisaidie kukubali mtazamo Wako wenye huruma unitakase kutokana na kila dhambi.  Kwa huruma Yako, Bwana mpendwa, ondoa dhambi maishani mwangu na kuweka Huruma Yako mahali pake.  Nami nisaidie nisikukimbie kamwe.  Yesu, nakutumainia.

Februari 2: Kutolewa Bwana Hekaluni—Sikukuu

Tafakari Zaidi juu ya Huruma ya Mungu

Tafakari za Kila Siku za Injili

Watakatifu/Sikukuu za Leo