Kiswahili

Tafakari 212: Kushinda Shaka

“Shaka” ni nini?  Kuwa na shaka ni kukosa imani, na kukosa imani ni kutoutumainia ufunuo mkamilifu na mpango mkamilifu wa Mapenzi ya Mungu.  Kwanza kabisa, shaka inayotokana na kukosa imani inamaanisha kwamba husikilizi.  Tunapokuwa na shaka juu ya Mungu, mpango Wake na yote anayotufunulia, sisi…

Tafakari ya 211: Karibu na Mama wa Mungu

Upendo wa mama unaweza kuelezwa kuwa “wenye nguvu” kwa maana kwamba angekuwa tayari kutoa uhai wake ili kuwalinda watoto wake.  Msukumo wa asili wa kimama huamka wakati mtoto wake yuko hatarini, anaumia, au ana uhitaji, naye husahau kabisa ustawi wake mwenyewe ili kumlinda…

Tafakari ya 210: Matendo Mema katika Mwanga wa Upendo wa Mungu

Je, unafanya kazi kwa bidii?  Je, unajitahidi kuwa mwema?  Je, unataka kuleta mabadiliko yenye manufaa?  Hakika ni vema kujitahidi kuwa mwema.  Lakini tunapofanya hivyo, hatupaswi kamwe kufikiri kwamba “wema” wetu ni mwema kweli machoni pa Mungu, isipokuwa Upendo wa Mungu ndio umekuwa chanzo…

Tafakari ya 209: Kushinda Mazoea ya Dhambi

Kushinda dhambi kunahitaji Huruma ya Mungu.  Mara nyingi mno tunajaribu kushinda dhambi kwa juhudi zetu wenyewe.  Hii ni kazi ya bure, kwa kuwa hutaweza kamwe kushinda dhambi yako kwa juhudi zako mwenyewe.  Kuna njia moja tu ya kujiondolea dhambi unayopambana nayo, nayo…

Tafakari ya 208: Mshale wa Kiroho wa Huruma

Kwa kawaida, mshale hujeruhi na kuua. Mishale imetumiwa katika historia yote kwa vita na kwa kuwinda. Lakini mshale wa kiroho wa Huruma ni tofauti sana. Kumbuka maneno ya nabii Simeoni aliyomwambia Mama yetu Mbarikiwa, “Na wewe mwenyewe upanga utakuchoma” (Luka 2:35). Na…

Tafakari ya 207: Kupata Faraja katika Moyo wa Kristo

Mara nyingi watoto hupata faraja kubwa wanapojibanza karibu na mzazi mwenye upendo na wororo.  Kuna uradhi mkubwa katika kukumbatiwa kwa nguvu na mikono hii yenye upendo.  Katika nyakati hizi, hofu na wasiwasi huondoka, na amani na kitulizo hurudi pale palipokuwa na dhiki.  Ndivyo inavyopaswa…

Tafakari ya 206: Kujilimbikizia Mambo ya Kiroho

Hatari halisi kwa maisha ya kiroho inaweza kuitwa “kujilimbikizia mambo ya kiroho.”  Hii ni hali ya mtu anayejaribu kujifanya mlengwa wa mwisho wa Huruma ya Mungu badala ya kuwa chombo cha Huruma ya Mungu.  Kwa kujaribu kuwa mlengwa wa mwisho wa Huruma ya Mungu, mtu…

Tafakari ya 205: Ngome ya Amani

Amani ya Bwana ni kama ngome ambamo tunapaswa kukimbilia ili kujikinga na mashambulizi yote ya nje yanayotoka kwa yule mwovu.  Nje ya ngome hii tunakuwa wazi kwa mashambulizi hayo yote yenye nia mbaya.  Mishale ya hasira, ukandamizaji, udanganyifu na wivu inaweza kutudhuru sana bila ulinzi mtakatifu…

Tafakari ya 204: Kikombe cha Nafsi Yako

Kikombe cha ua ni jani la nje linalozunguka petali zinazoanza kuumbika, likizilinda zinapokua. Kinafanyiza namna ya “kitalu” ambamo petali changa hukua. Zinapokua ndani ya mahali hapa palipofichika, kikombe cha ua huzilinda. Na zinapokomaa, kikombe cha ua hufunguka…

Tafakari ya 203: Kina na Upana wa Huruma

Fikiria ukipewa kazi ya kuhesabu kila chembe ya mchanga duniani. Bila shaka, hiyo ingekuwa kazi isiyowezekana. Kwa kweli, hata watu wote duniani kwa pamoja wasingeweza kuikamilisha kazi hiyo. Baadhi ya mambo yanazidi tu uwezo wetu. Kazi nyingine ambayo ingekuwa hata…