Kiswahili

Tafakari 318: Kutojali na Kusahau

Kama ungekuwa katika ndoa na mara kwa mara ukawa humjali mwenzi wako, hilo lingekuwa tatizo.  Kutojali maana yake ni kutokuwa na moyo wa kujali kwa dhati mema ya mwingine.  Kusahau ni dalili ya kutojali kwa kuwa mtu asipojali sana, ni rahisi kwake kusahau.  Kwa mfano…

Tafakari ya 317: Kuwahukumu Wengine

Ni rahisi sana kumhukumu mwingine, lakini ni vigumu sana kujizuia kufanya hivyo.  Kwa nini hali iko hivyo?  Kwa nini unaweza kujikuta ukiwahukumu wengine kwa urahisi ilhali kwa kweli hujui yaliyo mioyoni mwao?  Hakika kunaweza kuwa na sababu nyingi za dhambi hii; mojawapo…

Tafakari 311: Ukweli wa Unyenyekevu

Fadhila tukufu ya unyenyekevu inapaswa kueleweka, kutafakariwa daima na kukumbatiwa daima.  Unyenyekevu ni nini?  Si kingine ila kuujua ukweli kuhusu wewe mwenyewe, kuuamini ukweli huo na kuishi kulingana nao.  Ni wewe na Mungu tu mnaojua undani wa dhamiri yako.  Wanadamu…

Tafakari 241: Kutibu Dhambi Zako Mahususi

Unazishindaje dhambi zako?  Kila dhambi ni tofauti na inahitaji sala na sadaka mahususi ili ujitenge nayo.  Aina tatu za dhambi zilizo za kawaida ni: dhambi za mwili, dhambi za hasira na dhambi za kiburi.  Kila moja ya dhambi hizi inaweza kushindwa, lakini huenda ikahitaji uangalifu wa pekee…

Tafakari ya 157: Kufanya Maamuzi ya Kimaadili

Je, wakati mwingine unapata shida kufanya uamuzi ulio sahihi kimaadili? Hali hii hutokana na asili yetu ya kibinadamu iliyoanguka dhambini. Tunachanganyikiwa kwa urahisi maishani na tunaweza kushindwa kwa urahisi kufahamu Mawazo na Mapenzi ya Mungu. Basi ufanye nini? Jua kwamba dhamiri yako ni patakatifu ambapo…

Tafakari ya 58: Kutakaswa Dhambi

Dhambi ni mada ambayo watu wengi huiepuka.  Hatupendi kufikiria dhambi zetu.  Hatupendi kuzikiri, na mara nyingi tunazitafutia sababu za kuzihalalisha kana kwamba hatuna dhambi yoyote.  Tunaweza kwa urahisi kupata visingizio vya “dhambi” hii au ile.  Lakini hapa kuna mtazamo mwingine kuhusu dhambi.  Sisi…

Tafakari ya 49: Kutoeleweka

Tumeitwa kuwa watakatifu.  Na tukifuata njia hiyo, tutaitwa kuishi kwa fadhila za kishujaa.  Wengine hawataelewa daima fadhila za kishujaa.  Kwa kweli, kwa mtazamo wa hekima ya ulimwengu, fadhila za kishujaa na takatifu ni upumbavu.  Lakini hatupaswi kuruhusu…

Tafakari ya 352: Adhabu na Hisia ya Hatia

Huenda isiwe jambo la kupendeza kutafakari adhabu ya Mungu.  Lakini lazima ieleweke kwamba adhabu Zake ni halisi na ni tendo la Huruma Yake tele.  Nafsi zinapomwacha Mungu na kuikataa Huruma Yake, jambo hili linaujeruhi sana Moyo Wake.  Kwa sababu hiyo, Mungu anakuwa…