Kiswahili

Tafakari 329: Kuungama kwa Furaha

Kwa nini unaogopa kuungama?  Sakramenti hii tukufu unatolewa kutoka katika Moyo wenye huruma wa Bwana wetu.  Kwa njia ya zawadi hii tukufu, Yesu anakuondolea mizigo unayobeba ili uweze kushiriki kikamilifu zaidi katika Huruma Yake.  Kama ungeelewa hili…

Tafakari 304: Ukweli katika Mambo Yote

Je, tuuogope ukweli?  Kwa upande mmoja, ukweli unaweza kutuingiza matatizoni.  Kwa mfano, watazame Mashahidi.  Wao ni mashahidi wa ukweli kwa kumwaga damu yao.  “Waliingia matatizoni” kwa maana hii tu: ushuhuda wao wa ukweli uliwaletea mateso.  Lakini…

Tafakari 300: Kufunua Siri za Nafsi Yako

Kwa kweli, inafariji sana kuwa na mtu unayeweza kumfunulia yaliyo ndani kabisa ya nafsi yako.  Mtu wa namna hii unayemwamini ni baraka kubwa anapokuhakikishia utunzaji kamili wa siri, huruma na uelewa.  Kuzungumza hata kuhusu dhambi zako bila kusita…

Tafakari 284: Kuishi katika Wakati wa Sasa

Jaribu moja la kawaida ambalo wengi hukabili ni kuishi katika yaliyopita au katika yajayo, na kushindwa kuishi katika wakati wa sasa. Unaishi katika yaliyopita unapoendelea kutawaliwa na matukio, dhambi, maumivu, na mambo mengine ya zamani. Yaliyopita…

Tafakari 283: Kuishinda Dhambi

Ujumbe wa Huruma ya Mungu ni rahisi sana kiasi kwamba tunaweza kuukosa kwa urahisi, hata baada ya kutafakari kurasa nyingi za kitabu hiki au Shajara ya Mtakatifu Faustina.  Ukweli rahisi ambao ujumbe wa Huruma ya Mungu unapaswa kuwasilisha ni kwamba hatupaswi kuwa na hofu yoyote ile ya kukiri dhambi zetu…

Tafakari 277: Huruma ya Kuondoa Mvutano

Mvutano mara nyingi ni sehemu ya maisha.  Wengine hukabiliana na mvutano mwingi, mfadhaiko na hata hasira kali sana katika maisha yao ya kila siku.  Mwanzoni, hasira ya mtu mwingine inaweza kukufanya uwe macho kujilinda na kukujaribu uingiwe na hofu.  Hili ni itikio la kawaida.  Hasira ya mtu mwingine inaweza pia kukusukuma…

Tafakari 268: Kutafakari Kifo

Labda kufikiria kifo chako kunakutia hofu.  Huenda si jambo unalolitafakari mara nyingi sana.  Lakini ni neema kuweza kukitazama kifo chako bila kukikwepa na kwa matumaini kamili.  Na unaweza kufanya hivyo kwa matumaini kamili ikiwa tu maisha yako yako katika hali njema…

Tafakari 267: Haki au Huruma?

Inafaa kuzungumza kuhusu Haki ya Mungu na pia Huruma Yake.  Havipingani.  Haki Yake itatekelezwa kwa wale wanaokataa kutubu, kama ilivyotekelezwa kwa malaika waliokataa kumtumikia Mungu.  Lakini, kwa sasa, inafaa zaidi kusema kwamba Mungu ni Mwenye Huruma.  Kwa kweli…

Tafakari ya 263: Mungu kama Nahodha Wako katika Dhoruba

Jiwazie ukiwa mtoto mdogo katika mashua ndogo katikati ya bahari. Dhoruba inaanza, wala huwezi kuona nchi kavu upande wowote. Mawimbi yanakurusha na kukugeuza, yakifunika omo la mashua kila yanapoipiga, nawe unajiuliza utawezaje kupona. Sasa jiwazie kwamba baba yako…

Tafakari ya 207: Kupata Faraja katika Moyo wa Kristo

Mara nyingi watoto hupata faraja kubwa wanapojibanza karibu na mzazi mwenye upendo na wororo.  Kuna uradhi mkubwa katika kukumbatiwa kwa nguvu na mikono hii yenye upendo.  Katika nyakati hizi, hofu na wasiwasi huondoka, na amani na kitulizo hurudi pale palipokuwa na dhiki.  Ndivyo inavyopaswa…