Kiswahili

Tafakari 127: Kumpenda Mungu kwa Njia ya Utii

Unaitwa kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, akili yako yote, roho yako yote na nguvu zako zote.  Lakini unafanyaje hivyo?  Kumpenda Mungu kwa vitendo kunadhihirikaje katika maisha yetu?  Hatimaye, tunampenda Mungu kwa njia ya utii mtakatifu.  Ni lazima tuyatii mapenzi Yake ya kimungu kuliko kitu kingine chochote.  Labda…

Tafakari ya 125: Nafsi Inayojitoa Sadaka

Je, unajua kwamba Bwana wetu huwachagua watu fulani kwa ajili ya utume maalumu wa kuteseka?  Yeye huwachagua watu fulani, ambao ni wachache, ili wafanane Naye kwa ukamilifu zaidi katika mateso aliyoyapata hapa duniani bila kuwa na hatia.  Nafsi hizi takatifu huteseka kwa njia nyingi na mbalimbali.  Wao ni mwendelezo wa…

Tafakari ya 122: Kama Ungeweza Kuchagua

Kama ungeweza kuchagua kati ya utajiri wote wa ulimwengu na uhusiano wa karibu na wenye upendo na Yesu, ungechagua nini? Usijibu haraka mno. Huenda tukajua kwamba kumchagua Yesu ndilo jibu sahihi, lakini je, ungemchagua? Fikiria mamlaka na “uhuru” wa kidunia ambao unge…

Tafakari ya 121: Bustani ya Siri Ndani ya Moyo Wako

Fikiria kwamba nyumba yako ilikuwa na ua wa ndani, uliojificha, ambamo ulikuwa na bustani.  Hakuna aliyejua kuhusu bustani hii ya siri.  Palikuwa mahali ulipopanda, kulima, kufanya kazi kwa bidii, kupalilia na kuvuna.  Kisha mazao ya bustani hii yaligawiwa kwa siri kwa…

Tafakari 117: Eneo la Faragha la Moyo Wako

Baadhi ya masista na wamonaki huishi maisha ya kujitenga ndani ya mipaka ya eneo la faragha.  Hakuna anayeruhusiwa kuingia katika eneo hilo bila sababu ya msingi, isipokuwa awe mwanajumuiya hiyo ya imani. Wengine wanaweza kuingia tu kwa ruhusa ya mkuu wa jumuiya.  Huenda ikawa…

Tafakari ya 107: Kuifunua Nafsi Yako katika Ungamo

Mungu anatutumia mapadri Wake kuwa wawakilishi Wake.  Ingawa mapadri si wakamilifu, bado wao ni wawakilishi wa Mungu.  Hili ni kweli hasa katika Sakramenti ya Upatanisho.  Ni muhimu tuikaribie Sakramenti hiyo…

Tafakari ya 106: Kulala katika Kristo

Kila usiku, unapokwenda kulala, unaalikwa kulala katika neema na Huruma ya Bwana wetu.  Unaalikwa kupumzika mikononi Mwake ili upate nguvu mpya na uchangamfu.  Usingizi ni mfano wa sala na, kwa kweli, unaweza kuwa namna ya kusali.  Kupumzika ni kupumzika katika Mungu.  Kila…

Tafakari 105: Matokeo ya Mungu Kukaa Ndani Yetu

Ungejisikiaje ikiwa Mungu angekaa kikamilifu katika vilindi vya nafsi yako?  Amani, furaha na mshangao!  Na kutokana na zawadi hizi, na kutokana na Utatu Mtakatifu kukaa ndani yako, ungekuwa na ujasiri wa kukabili magumu, nguvu za kuondoa hofu na ulinzi usiopenyeka…

Tafakari ya 104: Rozari ya Huruma

Sala ni ya lazima katika safari yetu ya Kikristo.  Unaposali, ni vizuri kusema kutoka moyoni, ukimmiminia Mungu yaliyo moyoni mwako.  Lakini sala lazima pia iendane na imani yako na yote unayoyajua kumhusu Mungu.  Lazima ionyeshe ufahamu wako wa kweli kumhusu Mungu na kuomba Huruma Yake.  Rozari…

Tafakari 103: Kumjua Mungu Ni Zaidi ya Maneno

Ushirika na Utatu lazima uwe lengo kuu la maisha yetu.  Na ingawa tunaweza kuzungumza Nao kwa maneno, mawasiliano ya ndani kabisa ni zaidi ya maneno.  Ni muungano, ni kujitoa wenyewe na kufurahia Huruma Yao.  Kujua na kuzungumza…