Kiswahili

Tafakari ya 101: Mungu Akisema Kupitia Wengine

Mara nyingi sana, Mungu anataka kukupa ujumbe maalumu ambao unahitaji kuusikia.  Inaweza kutokea kwamba, unaposikiliza homilia, kusoma kitabu, kusikia jambo redioni au kuzungumza na rafiki, jambo fulani litavuta fikira zako kwa namna ya pekee ingawa halionekani kuwagusa…

Tafakari ya 100: Tamaa ya Kutenda Mema

Mungu hututabasamia na kutujalia thawabu tele kwa upendo tunaomwonyesha Yeye na wengine.  Matendo yetu ya upendo, yanapochochewa na neema Yake, hugeuzwa kuwa hazina Mbinguni.  Lakini si hayo tu yanayogeuzwa kuwa hazina.  Hata tamaa yetu ya kutenda mema…

Tafakari 99: Mjeledi wa Dhambi

Kwa nini Yesu aliteseka namna ile?  Kwa nini alipigwa mijeledi kwa ukali kiasi kile?  Kwa nini kifo Chake kilikuwa na maumivu makali kiasi kile?  Kwa sababu dhambi ina matokeo na ni chanzo cha maumivu makubwa.  Lakini Yesu kuyakubali mateso kwa hiari na bila dhambi kuliyageuza…

Tafakari ya 98: Kuwa Chombo

Mungu anapotuita kutimiza utume fulani, ni nani anayetenda kazi?  Mungu au sisi?  Ukweli ni kwamba sote tunatenda kazi: Mungu ndiye chanzo nasi ni chombo.  Tunajitahidi kwa hiari yetu, lakini ni Mungu anayeangaza kupitia sisi.  Kama vile dirisha linavyoweza kuwa chanzo cha mwanga…

Tafakari ya 97: “Kisingizio” cha Udhaifu Wetu

Ikiwa ungeombwa kujenga chombo cha kusafiria angani kinachoendeshwa kwa roketi kuanzia mwanzo, huenda ungepinga kwa kusema kwamba huna ujuzi katika eneo hilo na, kwa hiyo, huwezi kufanya unachoombwa kufanya.  Mara nyingi tunamjibu Mungu vivyo hivyo kuhusu Mapenzi Yake.  Ni rahisi kwetu kuhisi…

Tafakari 96: Mpango Mkuu Ambao Mungu Anao kwa Ajili Yako

Sote, nyakati fulani, tunaweza kuwa na ndoto za ukuu.  Ingekuwaje kama ningekuwa tajiri na maarufu?  Ingekuwaje kama ningekuwa na mamlaka makubwa katika ulimwengu huu?  Ingekuwaje kama ningekuwa Papa au Rais?  Lakini tunachoweza kuwa na hakika nacho ni kwamba kwa kweli Mungu ana mambo makuu aliyotupangia.  Anatuita kwenye ukuu…

Tafakari ya 95: Kuitumainia Huruma ya Mungu

Kama ungeangusha kitu katikati ya bahari pana sana, ungejua kwa hakika kabisa kwamba kitu hicho kingelowa.  Ukubwa wa bahari hiyo ungekimeza.  Ndivyo ilivyo Huruma ya Mungu.  Ni kuu mno na haina kikomo.  Kwa hiyo, ikiwa unatumaini…

Tafakari ya 94: Kumkabili Yule Mwovu

Ikiwa unataka kuepuka chuki kali ya yule mwovu, basi acha kujitahidi kuwa mtakatifu.  Shetani bado atakuchukia, lakini hatakuchukia kwa kadiri anavyomchukia mtakatifu.  Lakini, bila shaka, huu ni upumbavu!  Kwa nini mtu yeyote aepuke utakatifu ili aepuke chuki…

Tafakari ya 93: Makutano ya Upendo na Dhambi

Upendo na dhambi hukutana wapi?  Hukutana katika mateso, dhihaka na nia mbaya alizotendewa Bwana wetu.  Yeye alikuwa upendo mkamilifu uliojifanya mwili.  Huruma iliyokuwa katika Moyo Wake haikuwa na kikomo.  Kuwajali Kwake watu wote na kuhangaikia hali yao kulipita kila fikira.  Na bado askari walimdhihaki…

Tafakari ya 92: Ubunifu katika Sala

Mara nyingi, siku zetu hujaa shughuli.  Familia mara nyingi hujishughulisha na tukio hili au lile.  Shughuli za nyumbani na kazi zinaweza kurundikana, na mwisho wa siku tunaweza kugundua kwamba tumekuwa na muda mchache wa kusali kwa Mungu katika faragha.  Lakini tunaweza kupata faragha na kusali katika nyakati…