Kiswahili

Tafakari 220: Nafsi Inayoteseka

Baadhi ya watu huhisi mateso makali ndani kabisa ya nafsi zao.  Wakati mwingine hali hii husababishwa na dhambi, na wakati mwingine husababishwa na Huruma ya pekee ya Mungu inayoiwezesha nafsi kupata uzoefu wa mateso ambayo Yesu alipitia.  Hata iweje, ukipatwa na…

Tafakari ya 214: Msamaha Kamili

Fikiria kwamba ulikuwa na hatia ya uhalifu mkubwa na ulikabiliwa na kifungo cha maisha gerezani. Ulijuta kwa ulichofanya na ukakiri kosa lako kikamilifu. Siku ya kutolewa hukumu yako, uliletwa ukiwa umefungwa pingu kutoka mahali ulipokuwa ukishikiliwa, ukijua kwamba ungerudi huko muda si mrefu. Badala yake, hakimu…

Tafakari ya 209: Kushinda Mazoea ya Dhambi

Kushinda dhambi kunahitaji Huruma ya Mungu.  Mara nyingi mno tunajaribu kushinda dhambi kwa juhudi zetu wenyewe.  Hii ni kazi ya bure, kwa kuwa hutaweza kamwe kushinda dhambi yako kwa juhudi zako mwenyewe.  Kuna njia moja tu ya kujiondolea dhambi unayopambana nayo, nayo…

Tafakari ya 208: Mshale wa Kiroho wa Huruma

Kwa kawaida, mshale hujeruhi na kuua. Mishale imetumiwa katika historia yote kwa vita na kwa kuwinda. Lakini mshale wa kiroho wa Huruma ni tofauti sana. Kumbuka maneno ya nabii Simeoni aliyomwambia Mama yetu Mbarikiwa, “Na wewe mwenyewe upanga utakuchoma” (Luka 2:35). Na…

Tafakari ya 204: Kikombe cha Nafsi Yako

Kikombe cha ua ni jani la nje linalozunguka petali zinazoanza kuumbika, likizilinda zinapokua. Kinafanyiza namna ya “kitalu” ambamo petali changa hukua. Zinapokua ndani ya mahali hapa palipofichika, kikombe cha ua huzilinda. Na zinapokomaa, kikombe cha ua hufunguka…

Tafakari 200: Umoja wa Upendo na Mateso

Je, upendo na mateso vinapingana?  Kwa maneno mengine, ikiwa unahisi mateso mengi, je, unaweza pia kuwa na upendo mkubwa?  Swali moja la kutafakari ni hili: Chanzo cha mateso yako ni nini?  Je, ni dhambi yako?  Je, ni huruma kwa mtu mwingine?  Je, ni ya kimwili au ya kisaikolojia…

Tafakari ya 199: Umoja na Yesu ni Umoja na Wengine

Kanisa lina utukufu kwa sababu nyingi. Mojawapo ya mambo yenye utukufu katika Kanisa ni umoja uliomo ndani yake. Ni kweli kwamba nyakati fulani kuna migawanyiko mingi ndani yake, maumivu na machafuko ya kila aina. Lakini haya si sifa za Kanisa. Haya ni matokeo ya dhambi…

Tafakari ya 197: Nina Kiu

“Nina kiu.”  Maneno haya mawili rahisi yana maana kubwa sana.  Bwana wetu aliyatamka akiwa Msalabani.  Askari mmoja alijaribu kumpa faraja kwa kumpa sifongo iliyoloweshwa katika siki ya divai ili kumkata kiu.  Divai iliyogeuka siki ni ishara ya nafsi iliyogeuka…

Tafakari ya 191: Nafsi Inayopenda Kuzungumza Sana

Hamu iliyopitiliza ya kuzungumza ni hatari halisi kwa maisha ya ndani ya ushirika na Mungu.  La, kuzungumza si dhambi, na mara nyingi ni tendo la Huruma kwa mwingine.  Lakini kuna nyakati ambapo kuzungumza kupita kiasi huwa kizuizi kwa Huruma ya Mungu.  Kuzungumza, kwenyewe tu, si…

Tafakari ya 190: Uumbaji Wote Unampa Mungu Utukufu

Vitu vyote vimeumbwa kwa lengo moja la mwisho: kuusifu na kuutukuza Utatu Mtakatifu.  Tumeumbwa kwa lengo hili tu, si kwa lengo kubwa zaidi, dogo zaidi, wala jingine lolote.  Sisi wanadamu tumeitwa kumpa Mungu sifa na utukufu wa pekee kwa kumwabudu kupitia maisha…