Kiswahili

Tafakari 311: Ukweli wa Unyenyekevu

Fadhila tukufu ya unyenyekevu inapaswa kueleweka, kutafakariwa daima na kukumbatiwa daima.  Unyenyekevu ni nini?  Si kingine ila kuujua ukweli kuhusu wewe mwenyewe, kuuamini ukweli huo na kuishi kulingana nao.  Ni wewe na Mungu tu mnaojua undani wa dhamiri yako.  Wanadamu…

Tafakari ya 310: Upumbavu wa mwovu

Shetani yupo kweli na vishawishi vyake ni vya kweli.  Anakuchukia kwa chuki tupu na anatamani uangamie.  Ni vizuri kujua hili.  Lakini mwovu pia ni mjanja sana na anajua jinsi ya kukuhadaa, na ni nadra atakapokuambia uongo ulio wazi, kwa sababu anajua kwamba kuna uwezekano mkubwa kishawishi hiki hakitakushawishi…

Tafakari ya 309: Kuzungumza na Wengine

Tunapozungumza na mtu mwingine, daima tunapata fursa ya kushirikishana upendo wa Mungu.  Hata mazungumzo ya kawaida yanaweza kufanya hivyo.  Kwa mfano, kusikiliza kwa makini maelezo kuhusu maisha ya mwingine huonyesha kwamba unamjali na kumhangaikia, na hudhihirisha kwamba unatambua hadhi yake…

Tafakari ya 303: Ukimya

Mojawapo ya hatari ambazo watu wengi hukumbana nazo katika ulimwengu wetu wa kisasa wa kiteknolojia ni kelele zisizokoma.  Ni rahisi kuzingirwa na maneno mengi kutwa nzima.  Hayo yanaweza kutufikia kupitia redio, televisheni, Intaneti, au mazungumzo yasiyokoma ya mtu mwingine.  Ni nadra kupata nyakati za ukimya mkubwa…

Tafakari ya 302: Akili Pana, Yenye Nguvu na Wepesi wa Kuelewa

Akili zetu ni zawadi kutoka kwa Mungu na ni mojawapo ya njia mbili kuu ambazo kwazo tumeumbwa kwa sura na mfano Wake.  Njia nyingine ni kupitia zawadi ya utashi wetu huru.  Lakini akili ni zawadi ya ajabu ambayo lazima itolewe kwa ajili ya kazi ya Mungu.  Ni vizuri kusali ili Bwana wetu…

Tafakari ya 301: Ushirika wa Watakatifu

Jambo moja linalopaswa kutuhamasisha kufanya kazi kwa bidii katika kueneza Huruma ya Mungu ni uhalisi wa Ushirika wa Watakatifu.  Kuuelewa ushirika huu wa milele kutatuwezesha kutambua kwamba yale tunayofanya sasa tutayafurahia milele Mbinguni.  Kwa mfano, ikiwa…

Tafakari 299: Uchovu wa Hekima ya Kibinadamu

Maneno ya ukweli, yanayotoka katika Moyo wa Bwana wetu, huleta furaha katika maisha yetu na kuzipa roho zetu nguvu mpya.  Unapoyasikia maneno haya ya ukweli, kuyapokea moyoni na kuyatenda, unawekwa huru kutoka katika mzigo wa upotovu na unaweza kuhisi unafuu na kuburudika rohoni.  Hata hivyo…

Tafakari ya 293: Kushushwa Hadi Kuwa Si Kitu

Je, unaona thamani ya kushushwa hadi kuwa si kitu machoni pako mwenyewe?  Huenda huioni.  Sababu ya lugha hii kuwa ngumu kukubalika ni kwamba unyenyekevu unaeleweka kikamilifu tu kwa kipawa maalumu cha neema ya Mungu.  Baadhi ya wanafalsafa wa kale hata huitukuza kiburi kama fadhila kuu, wakipuuza…

Tafakari ya 289: Shauku kwa Roho za Watu

Unapoitazama shauku iliyo moyoni mwako, ni nini kinachojitokeza zaidi?  Bila shaka kuna mambo mengi yanayokuvutia.  Thawabu na raha nyingi za kidunia zinaweza kwa urahisi kutawala matamanio yako.  Hamu ya raha za mwili, fedha na mafanikio ya kidunia ni miongoni mwa shauku zenye nguvu zaidi kwa…