Kiswahili

Tafakari 182: Hekima ya Kupenya Siri za Kiburi

Kiburi kinaweza kututawala kabisa.  Hilo linapotokea, tunachofikiria tu ni sisi wenyewe na uchungu wetu.  Labda unaelewa hali hii kutokana na uzoefu wako.  Huenda umejeruhiwa moyoni, nawe unakaa ukinuna kwa sababu ya jeraha hilo.  Linatia uchungu moyoni mwako, nawe unatafuta kuliponya.  Lakini…

Tafakari 181: Kutofungamana Kutakatifu

Je, inajalisha Mapenzi ya Mungu kwako ni yapi?  Mwanzoni, huenda swali hilo likasikika kuwa la ajabu.  Lakini litafakari.  Je, inajalisha Mungu anataka nini kutoka kwako?  Ingekuwaje kama angekuita kufanya kazi daima?  Au kama angekuita kupumzika kwa utulivu?  Au…

Tafakari ya 180: Mateso ya Yesu

Sisi tuliozoea Injili huenda nyakati fulani tukapatwa na hali fulani ya kutojali mateso ya Kristo.  Tunasikia simulizi hilo likisomwa kila mwaka, tumeona picha nyingi za Mateso Yake, na kwa sababu ya kuyazoea, tunaweza kushindwa kuyaruhusu yawe na athari inayostahili…

Tafakari 179: Kukabiliana na Ukiwa wa Ndani

“Bwana hutoa na Bwana hutwaa…” (Ayubu 1:21). Maneno haya ni ya kweli kabisa. Kuna nyakati maishani tunapopata faraja tele kutoka kwa Mungu. Huenda ikawa wakati wa furaha kubwa katika familia, au tunapopata upendo usio na masharti kutoka kwa mtu mwingine. Wakati…

Tafakari 178: Utakatifu Haupatikani Kamwe kwa Nguvu Zetu Pekee

Je, unatamani kuishi maisha matakatifu?  Ikiwa ndivyo, huwezi kufanya hivyo kwa nguvu zako pekee.  Unahitaji msaada wa mtu mwingine, na hata wa watu wengine wengi.  Bwana ametupatia njia nyingi za kuongozwa kwa upendo na wengine.  Baadhi wamejaliwa kuwa na kiongozi wa kiroho wa miaka mingi…

Tafakari 177:  Utii Mtakatifu

Mojawapo ya kinga kuu dhidi ya kufanya mapenzi yetu wenyewe badala ya yale ya Mungu ni utii mtakatifu.  Wale walio katika maisha ya kitawa wamebarikiwa kuuishi utii huu kwa namna halisi na ya nje, wakiruhusu zoea hilo la nje liingie ndani ya mioyo yao ili wawe na hakika kwamba wanaishi…

Tafakari 176:  Kupambana na Dhambi ya Ulimwengu

Mungu anapoutazama ulimwengu, anaona nini?  Bila shaka anaona uzuri wa uumbaji Wake, mpangilio mkamilifu wa kusudi Lake na uwepo wa wana na binti Zake.  Lakini pia anaona ubaya wa kutisha wa wingi wa dhambi.  Hata dhambi ndogo kabisa…

Tafakari 173: Umoja na Mmoja ni Umoja na Watatu

Utatu Mtakatifu huelezwa kuwa na asili moja ya kimungu, huku ukiwa Nafsi tatu zilizo tofauti.  Hivyo, Nafsi hizo tatu zilizo tofauti zinashiriki umoja mkamilifu.  Kwa kweli, zisingeweza kuwa “zimeungana” kama zisingekuwa tofauti kila moja na nyingine.  Kwa hiyo ni lazima kusema…

Tafakari 168: Kuomba Huruma ya Mungu kwa Ajili ya Wengine

Kuna jambo moja, na moja tu, lenye uwezo wa kuwaokoa wenye dhambi kutoka katika moto wa jehanamu.  Jambo hilo ni Huruma.  Mungu hutoa Huruma Yake bure na kwa wingi, lakini pia amechagua kutoa Huruma Yake akiitikia sala zetu tunaposali kwa…

Tafakari ya 166: Nguvu ya Umoja Wako na Kristo

Fikiria ukiwa Mweza wa Yote, au ukiwa rafiki wa karibu wa yule aliye Mweza wa Yote. Kuna simulizi kuhusu Papa Mtakatifu Leo I, aliyeishi katika karne ya tano, linalodhihirisha nguvu ya Mungu. Inasemekana kwamba Attila Mhuni na jeshi lake lenye ukatili walitaka kuiteka na kuipora Roma. Papa Mtakatifu Leo…