Kiswahili

Tafakari ya 42: Kutendewa Isivyo Haki Kunakotolewa kama Fidia ya Dhambi

Mara nyingi maishani tunatendewa isivyo haki.  Kwa hiyo, msukumo wetu wa kwanza ni kupambana na wanaotutendea hivyo, kujitetea na kuhakikisha kwamba haki inatendeka.  Lakini je, hivyo ndivyo Yesu alivyofanya?  La, alinyamaza na kukubali dhuluma zote kama sadaka ya kufidia dhambi zetu.  Alikuwa yule…

Tafakari 40: Kuingia ndani ya Moyo wa Bwana Wetu

Chembe ya vumbi au punje ya mchanga huwa haina umuhimu mkubwa katika hali nyingi.  Hakuna anayetambua chembe moja au punje moja uani au hata sakafuni ndani ya nyumba.  Lakini mojawapo ikiingia jichoni, punje au chembe hiyo hutambulika mara moja.  Kwa nini?  Kwa sababu…

Tafakari 39: Kupoteza Faraja ya Kiroho

Ni rahisi kuingia katika mtego wa kufikiri kwamba, kwa sababu tunamfuata Yesu, tunapaswa kufarijiwa na kutiwa moyo daima katika yote tunayofanya.  Je, hiyo ni kweli?  Ndiyo na hapana.  Kwa maana fulani, faraja yetu itadumu ikiwa daima tunatimiza Mapenzi ya Mungu na tunajua kwamba tunayatimiza.  Hata hivyo…

Tafakari ya 38: Wajibu Wetu wa Kila Siku

Huenda wengine wakahisi kwamba maisha yao hayana uchangamfu na ni ya kurudiarudia mambo yaleyale.  Ni mambo yaleyale siku baada ya siku. Wakati mwingine tunatafuta mambo mapya ya kutusisimua na uzoefu mpya.  Lakini tukiruhusu neema iandamane nasi kila siku, katika mambo ya kawaida ya maisha yanayojirudia na yasiyo na uchangamfu…

Tafakari ya 37: Unyenyekevu, Usahili na Unyofu

Kuna maneno matatu ya kutafakari leo: unyenyekevu, usahili na unyofu. Watu wanyenyekevu humwona na kumjua Mungu kwa sababu hawajitegemei wenyewe wanapokuwa na uhitaji. Wanatambua kwamba Mungu ndiye kila kitu na kwamba, bila Yeye, wao si kitu. Watu wenye usahili hawanaswi…

Tafakari ya 36: Huruma ya Urafiki wa Kiroho

Wakati mwingine tunahisi kwamba maisha ni magumu.  Maisha yetu ya kiroho yanaweza kuonekana kuwa na ukavu au kutulemea.  Dhambi zetu zinaweza kuonekana kuwa nyingi mno hata tushindwe kuzishinda.  Na uhusiano wetu na Mungu unaweza kuonekana kuwa mgumu mno kuukuza.  Lakini hali hizi zote ni neema ambazo…

Tafakari ya 34: Kutosheka Katika Mungu Pekee

Mara nyingi maishani tunaweza kuangukia katika mtego wa kuamini kwamba vitu vya kidunia vinavyopita vinatutosheleza. Tunaweza hata kudanganyika na kufikiri kwamba dhambi zetu zinatutosheleza. Na, kwa namna ya ajabu, kwa kiasi fulani zinatupa hali ya kutosheka kwa muda. Lakini hali hii ya “kutosheka” ni…

Tafakari ya 30: Kumtii Mungu

Utii ni ufunguo mmoja wa utakatifu.  Adamu na Hawa walipoteza neema kwa kutotii, nasi tunarudishiwa neema kwa kutii.  Utii unaweza kuwa mgumu na unahitaji uamuzi wa dhati kutoka ndani ya moyo.  Tafuta fursa za kumtii Yesu, hasa wakati wewe…

Tafakari ya 24: Utakaso wa Nafsi Yako

Mateso makubwa zaidi tunayoweza kustahimili ni shauku ya kiroho ya kuwa na Mungu.  Walioko toharani wanateseka sana kwa sababu wanamtamani Mungu na bado hawajawa Naye kikamilifu.  Ni lazima tuingie katika utakaso huohuo hapa na sasa.  Ni lazima tujiruhusu kumtamani Mungu.  Sisi…

Tafakari ya 18: Huruma Inayotolewa Kupitia Mapadri

Huruma hutolewa kwa njia nyingi. Kati ya njia nyingi za Huruma, itafute kupitia mapadri watakatifu wa Mungu. Mruhusu padri Wake akusikilize, azungumze nawe na akuongoze. Mapadri ni dhaifu na ni wenye dhambi. Lakini katika udhaifu wao wanapewa neema ya pekee ya kuongoza roho. …