Kiswahili

Tafakari 330: Kuwaombea Wengine

Usidharau nguvu ya sala zako.  Kadiri unavyozidi kutumainia Huruma ya Mungu, ndivyo sala zako zitakavyokuwa na nguvu zaidi kwa wale wanaozihitaji.  Bwana anajua mambo yote, naye anajua kila mtu anahitaji nini.  Lakini anataka kugawa neema Yake…

Tafakari ya 310: Upumbavu wa mwovu

Shetani yupo kweli na vishawishi vyake ni vya kweli.  Anakuchukia kwa chuki tupu na anatamani uangamie.  Ni vizuri kujua hili.  Lakini mwovu pia ni mjanja sana na anajua jinsi ya kukuhadaa, na ni nadra atakapokuambia uongo ulio wazi, kwa sababu anajua kwamba kuna uwezekano mkubwa kishawishi hiki hakitakushawishi…

Tafakari ya 292: Thamani ya Miito Maalumu

Baadhi ya watu wameitwa kuishi maisha ya pekee ya sala na upweke ndani ya maisha ya kitawa.  Hasa, kuna walioitwa kuishi maisha ya uheremiti au ya klauzura.  Watu hawa watakatifu wamejitenga na ulimwengu na hutumia siku zao katika sala ya kimya na kazi.  Lakini…

Tafakari 287: Joho la Fedheha

“Fedheha” inaweza kumaanisha aibu mbele ya watu, kuvunjiwa heshima, kudhalilishwa na kuona haya. Lakini neno hili huwa na maana ya pekee linapotumika kumhusu Yesu. “Joho la fedheha” linarejelea udhalilishaji ambao Yesu aliuvumilia mbele ya watu kwa sababu ya Msalaba Wake. Alihukumiwa kuwa mwenye dhambi na mwongo. Alishtakiwa kwa kuwadanganya watu na kujaribu kudhoofisha mamlaka za serikali. Alikuwa mlengwa…

Tafakari 283: Kuishinda Dhambi

Ujumbe wa Huruma ya Mungu ni rahisi sana kiasi kwamba tunaweza kuukosa kwa urahisi, hata baada ya kutafakari kurasa nyingi za kitabu hiki au Shajara ya Mtakatifu Faustina.  Ukweli rahisi ambao ujumbe wa Huruma ya Mungu unapaswa kuwasilisha ni kwamba hatupaswi kuwa na hofu yoyote ile ya kukiri dhambi zetu…

Tafakari ya 282: Mateso, Dhuluma, Unyanyasaji na Fedheha

Huenda kichwa hiki kisikuvutie mara moja.  Nani angetaka kuyavumilia mambo haya?  Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba Yesu aliyavumilia yote kwa kiwango cha juu kabisa.  Je, Yesu alikuwa na furaha?  Je, nafsi Yake ilikuwa na amani?  Bila shaka kabisa.  Hili linatufunulia…

Tafakari 281: Mapenzi ya Mungu Yasiyobadilika

Nyakati fulani, tunapompenda Mungu kwa upendo wa kina, tunaweza kujikuta tukisukumwa sana kufanya mambo makubwa kwa ajili Yake. Hata hivyo, licha ya hamu yetu na azimio letu thabiti, inaweza kuonekana kana kwamba Mungu haruhusu kazi yetu kusonga mbele. Huenda hii ni kwa sababu Bwana…

Tafakari 270: Vipengele vya Mapenzi ya Mungu

Je, uko tayari kuyakubali Mapenzi ya Mungu katika maisha yako?  Ikiwa ndivyo, lazima uwe tayari kupokea kila kipengele chake.  Mapenzi ya Mungu si wazo la jumla lenye ukuu wa kuvutia tu.  Kuyachagua Mapenzi Yake si kusema tu kwamba unachagua kumfuata kwa ujumla.  Badala yake, kuyachagua Mapenzi Yake…

Tafakari 267: Haki au Huruma?

Inafaa kuzungumza kuhusu Haki ya Mungu na pia Huruma Yake.  Havipingani.  Haki Yake itatekelezwa kwa wale wanaokataa kutubu, kama ilivyotekelezwa kwa malaika waliokataa kumtumikia Mungu.  Lakini, kwa sasa, inafaa zaidi kusema kwamba Mungu ni Mwenye Huruma.  Kwa kweli…

Tafakari 266: Kuvunjika Moyo Mbele ya Utakatifu

Je, unataka kuwa mtakatifu? Tunatumaini jibu ni “Ndiyo.” Lakini vipi kuhusu swali hili: Je, unafikiri unaweza kuwa mtakatifu? Huenda ikawa vigumu zaidi kujibu swali hili. Ni rahisi kuota kuhusu utakatifu na kutamani…