Kiswahili

Tafakari 330: Kuwaombea Wengine

Usidharau nguvu ya sala zako.  Kadiri unavyozidi kutumainia Huruma ya Mungu, ndivyo sala zako zitakavyokuwa na nguvu zaidi kwa wale wanaozihitaji.  Bwana anajua mambo yote, naye anajua kila mtu anahitaji nini.  Lakini anataka kugawa neema Yake…

Tafakari 329: Kuungama kwa Furaha

Kwa nini unaogopa kuungama?  Sakramenti hii tukufu unatolewa kutoka katika Moyo wenye huruma wa Bwana wetu.  Kwa njia ya zawadi hii tukufu, Yesu anakuondolea mizigo unayobeba ili uweze kushiriki kikamilifu zaidi katika Huruma Yake.  Kama ungeelewa hili…

Tafakari 300: Kufunua Siri za Nafsi Yako

Kwa kweli, inafariji sana kuwa na mtu unayeweza kumfunulia yaliyo ndani kabisa ya nafsi yako.  Mtu wa namna hii unayemwamini ni baraka kubwa anapokuhakikishia utunzaji kamili wa siri, huruma na uelewa.  Kuzungumza hata kuhusu dhambi zako bila kusita…

Tafakari 244: Kufanya Kazi Hadi Mwisho wa Dunia

Ikiwa unajitahidi, usiku na mchana, kueneza matendo ya Mungu, hilo ni jambo jema.  Matunda mema yatatokana na kujitoa kwako kutimiza Mapenzi ya Mungu na kueneza Huruma Yake ya Kimungu.  Lakini tunapaswa pia kutambua kwamba Mungu anaweza kututumia kueneza Huruma Yake hadi mwisho wa dunia.  Kwa namna gani?  Pekee…

Tafakari 184: Huruma katika Huduma ya Mapadre

La, mapadre si wakamilifu.  Wanatenda dhambi siku baada ya siku.  Wanahitaji daima kutubu na kuongoka katika maisha yao ya kila siku, kama wanadamu wengine wote.  Lakini wao ni mapadre.  Na kwa sababu ya upadrisho wao mtakatifu, Bwana huzungumza kupitia kwao kwa njia iliyo wazi…

Tafakari 177:  Utii Mtakatifu

Mojawapo ya kinga kuu dhidi ya kufanya mapenzi yetu wenyewe badala ya yale ya Mungu ni utii mtakatifu.  Wale walio katika maisha ya kitawa wamebarikiwa kuuishi utii huu kwa namna halisi na ya nje, wakiruhusu zoea hilo la nje liingie ndani ya mioyo yao ili wawe na hakika kwamba wanaishi…

Tafakari 108: Sauti ya Kanisa

Mungu amesema na watakatifu kwa njia nyingi, ikiwa ni pamoja na kupitia neema nyingi za ndani na misukumo ya kiroho.  Lakini hata mwanafumbo mkuu kuliko wote, aliye katika kilele cha utakatifu, hatimaye lazima aitii Sauti ya Mungu inayosema kupitia Kanisa Lake.  Kanisa, hasa…

Tafakari ya 107: Kuifunua Nafsi Yako katika Ungamo

Mungu anatutumia mapadri Wake kuwa wawakilishi Wake.  Ingawa mapadri si wakamilifu, bado wao ni wawakilishi wa Mungu.  Hili ni kweli hasa katika Sakramenti ya Upatanisho.  Ni muhimu tuikaribie Sakramenti hiyo…

Tafakari ya 18: Huruma Inayotolewa Kupitia Mapadri

Huruma hutolewa kwa njia nyingi. Kati ya njia nyingi za Huruma, itafute kupitia mapadri watakatifu wa Mungu. Mruhusu padri Wake akusikilize, azungumze nawe na akuongoze. Mapadri ni dhaifu na ni wenye dhambi. Lakini katika udhaifu wao wanapewa neema ya pekee ya kuongoza roho. …