Kiswahili

Tafakari 324: Wakati Unaotamaniwa Sana

Unatamani nini maishani?  Ikiwa ungeweza kuchagua jambo moja unalolitamani kuliko mengine yote, lingekuwa lipi?  Je, lingekuwa kifo?  Huenda sivyo.  Kwa kushangaza, huenda mtakatifu aliye mkuu kuliko wote angetamani kifo kuliko kitu kingine chochote maishani.  Si kifo cha mapema wala kifo cha kujichagulia mwenyewe; bali…

Tafakari 283: Kuishinda Dhambi

Ujumbe wa Huruma ya Mungu ni rahisi sana kiasi kwamba tunaweza kuukosa kwa urahisi, hata baada ya kutafakari kurasa nyingi za kitabu hiki au Shajara ya Mtakatifu Faustina.  Ukweli rahisi ambao ujumbe wa Huruma ya Mungu unapaswa kuwasilisha ni kwamba hatupaswi kuwa na hofu yoyote ile ya kukiri dhambi zetu…

Tafakari ya 271: Kutazama Zaidi ya Vikwazo vya Maisha

Mwelekeo na kishawishi kimoja kilicho cha kawaida sana ambacho watu wengi hupambana nacho ni kukazia fikira mateso, fedheha na maoni potofu ya wengine.  Tunapopatwa na mojawapo au zaidi ya mizigo hii, tunaweza kushawishika kuifanya kuwa kiini cha maisha yetu.  Kwa mfano…

Tafakari ya 232: Kuituliza Dhoruba

Kumbuka simulizi la Yesu akiituliza dhoruba (Mathayo 8:23-27).  Tendo hili la kimiujiza lilifanywa kama ishara ya kinabii ya Yeye kukuletea amani wakati wa changamoto mahususi unazokabiliana nazo maishani…

Tafakari 187: Upinde wa Mvua baada ya Dhoruba

Inastaajabisha jinsi uumbaji wenyewe unavyotangaza utukufu wa Mungu na kutufundisha mambo ya imani. Chukua mfano wa upinde wa mvua. Unang’aa na unapendeza, una rangi nyingi na unatia mshangao. Kila mtu hufurahi anapoona upinde wa mvua. Lakini upinde wa mvua usingekuwapo bila mvua au dhoruba. Ndivyo yalivyo maisha. Sisi…

Tafakari ya 171: Kulinganisha Dunia na Mbingu

Jaribu kuwazia utakavyofikiri kuhusu kipindi hiki cha maisha yako duniani utakapofika Mbinguni.  Je, utayatamani maisha haya?  Je, utataka kurudi?  Je, utatamani ungekuwa umepata fedha zaidi ulipokuwa hapa au ungekuwa na mafanikio zaidi ya kidunia?  Yaelekea sana kwamba hutafanya hivyo.  Ikilinganishwa na Mbingu, dunia hii inasikitisha.  Hilo halimaanishi…

Tafakari 156: Bwana Ndiye Kimbilio Letu

Kuna nyakati maishani ambapo hofu inakuingia.  Huenda una jukumu gumu linalokukabili, au unatembea katika njia usiyoijua.  Hali hizi, pamoja na mambo mengine mengi tunayopitia maishani, zinaweza kusababisha hofu na mahangaiko.  Hofu ya mambo usiyoyajua inaweza…

Tafakari ya 115: Mapenzi ya Mungu Yatakuhifadhi Salama

Mapenzi ya Mungu ni zaidi sana ya mpango wa siku zijazo ambao Mungu amekuandalia.  Ni zaidi ya matumaini na ndoto Zake kwa ajili yako.  Mapenzi Yake ndiyo njia yako ya kuelekea utakatifu, nayo ni chemchemi ya faraja na furaha kuu.  Mapenzi Yake yana namna ya kutenda na pia ya kutotenda (kuruhusu).  Ni…

Tafakari ya 86: Kuyeyusha Mioyo Migumu Zaidi

Wazia kipande kikubwa cha barafu.  Sasa wazia kwamba kuna sarafu yenye thamani katikati ya kipande hicho.  Ili kuipata sarafu hiyo, barafu hiyo lazima iyeyuke.  Hali inaweza kuwa hivyo pia kwa mioyo yetu.  Baadhi ya mioyo imekuwa migumu sana kadiri muda ulivyopita, kiasi kwamba uwezekano unaonekana kuwa mdogo…

Tafakari 54: Kuwaombea Wengine

Ni rahisi kudhani kwamba kila mtu tunayemjua ataenda Mbinguni.  Bila shaka, haya yanapaswa kuwa matumaini yetu.  Lakini ili mtu afike Mbinguni, lazima kuwe na wongofu wa kweli wa ndani.  Kila mtu anayeingia Mbinguni yuko huko kwa sababu ya uamuzi wake binafsi wa kumkabidhi Kristo maisha yake na kuiacha dhambi.  Jinsi gani…