Kiswahili

Tafakari 305: Kina cha Upendo wa Mungu

Fikiria mtu akitoa uhai wake kwa ajili yako kwa sababu anakupenda.  Alijikuta katika hali ambayo alijua kwamba ungepoteza uhai wako kama asingetoa wake kwa hiari.  Kwa hiyo, alichagua kujitokeza kwa ujasiri, akitoa uhai wake badala ya wako.  Ili…

Tafakari ya 208: Mshale wa Kiroho wa Huruma

Kwa kawaida, mshale hujeruhi na kuua. Mishale imetumiwa katika historia yote kwa vita na kwa kuwinda. Lakini mshale wa kiroho wa Huruma ni tofauti sana. Kumbuka maneno ya nabii Simeoni aliyomwambia Mama yetu Mbarikiwa, “Na wewe mwenyewe upanga utakuchoma” (Luka 2:35). Na…

Tafakari 201: Usiku pamoja na Yesu Gerezani

Wazia ingekuwaje kama ungeweza kwa namna fulani kupelekwa kwa njia ya kifumbo hadi usiku wa Alhamisi Kuu.  Na wazia kama ungeweza kwa namna fulani kuona na kupitia yote ambayo Yesu alipitia.  Wazia uchungu Wake bustanini, dhihaka na kutendewa kwa ukatili…

Tafakari ya 197: Nina Kiu

“Nina kiu.”  Maneno haya mawili rahisi yana maana kubwa sana.  Bwana wetu aliyatamka akiwa Msalabani.  Askari mmoja alijaribu kumpa faraja kwa kumpa sifongo iliyoloweshwa katika siki ya divai ili kumkata kiu.  Divai iliyogeuka siki ni ishara ya nafsi iliyogeuka…

Tafakari 142: Amani ya Bwana Huondoa Uovu

Ni muhimu kutambua kwamba mwovu, shetani, yupo.  Pia ni muhimu kutambua hasira na chuki yake.  Chuki yake ni kali kuliko tunavyoweza kuelewa.  Hana uwezo wa kuacha kutuchukia na kutafuta kutuangamiza kwa nguvu zake zote.  Kwa nini ni…

Tafakari 137: Nguvu katika Msalaba

Unaposali, je, wakati mwingine huketi na kuukazia macho msalaba wenye sanamu ya Yesu?  Kwa mtazamo wa mtu wa nje, msalaba huo ni jambo la kutatanisha.  Kwa nini tuinulie juu na kuheshimu tukio la kutisha namna hiyo?  Huenda mwanzoni mauaji ya kikatili ya Mwana wa Mungu yasiwe jambo linalotuvutia.  Hata hivyo…

Tafakari ya 70: Kujiona katika Kristo Anayeteseka

Ni taswira ipi ya Kristo inayokufanya ujisikie huru zaidi?  Ni taswira ipi ambayo unajiona ndani yake kwa urahisi zaidi?  Taswira ya Kristo aliyetukuzwa kama Mfalme wa wote?  Au taswira ya Kristo aliyepigwa na anayeteseka?  Mwishowe, tutamkazia macho Bwana katika utukufu na fahari, na hili litakuwa…

Tafakari ya 53: Magumu katika Sala

Tunakumbana na magumu ya ndani na ya nje tunapojitahidi kujenga mazoea ya kusali kila siku.  Magumu ya ndani: kuvunjika moyo, ukavu wa kiroho, uzito wa rohoni na vishawishi.  Magumu haya yanashindwa kwa subira na ustahimilivu.  Magumu ya nje…

featured image DM

Tafakari ya 5: Ukombozi wa Ulimwengu

Umwilisho ulikuwa tendo kuu zaidi la Huruma kuwahi kujulikana. Tendo pekee lililofuata na kulizidi lilikuwa tendo la Yesu kufa Msalabani, akiangamiza dhambi na mauti kwa damu Yake. Ukombozi wa ulimwengu kwa damu ya Msalaba ni tendo la upendo na Huruma…