Kiswahili

Tafakari 220: Nafsi Inayoteseka

Baadhi ya watu huhisi mateso makali ndani kabisa ya nafsi zao.  Wakati mwingine hali hii husababishwa na dhambi, na wakati mwingine husababishwa na Huruma ya pekee ya Mungu inayoiwezesha nafsi kupata uzoefu wa mateso ambayo Yesu alipitia.  Hata iweje, ukipatwa na…

Tafakari 218: Kumtambua Mungu Mara Moja Tu

Ni muhimu kumwelewa Mungu na njia Zake, lakini kuelewa si sawa na kujua.  Kumjua Mungu kunamaanisha kukutana na Nafsi.  Hatuishii tu kuelewa yale ambayo Nafsi hii inasema; bali tunawasiliana Naye, tunakutana Naye, tunapata mang’amuzi Yake na kuingia katika uhusiano Naye.  Kwa kweli…

Tafakari 217: Nafsi Yenye Uvivu Isiyojishughulisha

Tunamfurahisha yule mwovu tunapoziruhusu nafsi zetu kuwa na uvivu na kutokujishughulisha na mambo ya Mungu.  Nafsi isiyojishughulisha ni ile ambayo haitafuti kushiriki katika uzima wa Mungu.  Nafsi isiyojishughulisha ni ile ambayo haichukui hatua katika mambo ya kiroho badala ya kujishughulisha nayo.  “Kutochukua hatua” kunamaanisha kwamba mtu huyo…

Tafakari ya 210: Matendo Mema katika Mwanga wa Upendo wa Mungu

Je, unafanya kazi kwa bidii?  Je, unajitahidi kuwa mwema?  Je, unataka kuleta mabadiliko yenye manufaa?  Hakika ni vema kujitahidi kuwa mwema.  Lakini tunapofanya hivyo, hatupaswi kamwe kufikiri kwamba “wema” wetu ni mwema kweli machoni pa Mungu, isipokuwa Upendo wa Mungu ndio umekuwa chanzo…

Tafakari ya 209: Kushinda Mazoea ya Dhambi

Kushinda dhambi kunahitaji Huruma ya Mungu.  Mara nyingi mno tunajaribu kushinda dhambi kwa juhudi zetu wenyewe.  Hii ni kazi ya bure, kwa kuwa hutaweza kamwe kushinda dhambi yako kwa juhudi zako mwenyewe.  Kuna njia moja tu ya kujiondolea dhambi unayopambana nayo, nayo…

Tafakari ya 207: Kupata Faraja katika Moyo wa Kristo

Mara nyingi watoto hupata faraja kubwa wanapojibanza karibu na mzazi mwenye upendo na wororo.  Kuna uradhi mkubwa katika kukumbatiwa kwa nguvu na mikono hii yenye upendo.  Katika nyakati hizi, hofu na wasiwasi huondoka, na amani na kitulizo hurudi pale palipokuwa na dhiki.  Ndivyo inavyopaswa…

Tafakari ya 205: Ngome ya Amani

Amani ya Bwana ni kama ngome ambamo tunapaswa kukimbilia ili kujikinga na mashambulizi yote ya nje yanayotoka kwa yule mwovu.  Nje ya ngome hii tunakuwa wazi kwa mashambulizi hayo yote yenye nia mbaya.  Mishale ya hasira, ukandamizaji, udanganyifu na wivu inaweza kutudhuru sana bila ulinzi mtakatifu…

Tafakari ya 204: Kikombe cha Nafsi Yako

Kikombe cha ua ni jani la nje linalozunguka petali zinazoanza kuumbika, likizilinda zinapokua. Kinafanyiza namna ya “kitalu” ambamo petali changa hukua. Zinapokua ndani ya mahali hapa palipofichika, kikombe cha ua huzilinda. Na zinapokomaa, kikombe cha ua hufunguka…

Tafakari ya 197: Nina Kiu

“Nina kiu.”  Maneno haya mawili rahisi yana maana kubwa sana.  Bwana wetu aliyatamka akiwa Msalabani.  Askari mmoja alijaribu kumpa faraja kwa kumpa sifongo iliyoloweshwa katika siki ya divai ili kumkata kiu.  Divai iliyogeuka siki ni ishara ya nafsi iliyogeuka…

Tafakari ya 195: Furaha Yetu Tamu

Kama ungekuwa mtaalamu wa kuonja divai, na ungekuwa na nafasi ya kuchagua kati ya chupa ya divai bora na ile ya bei rahisi, bila shaka ungechagua ile bora.  Ungejua tofauti yake, wala usingepata furaha kubwa katika divai ya bei rahisi ukijua…