Kiswahili

Tafakari 148: Huruma kwa Walio Toharani

Mpendwa wetu anapofariki, ni rahisi kudhani mara moja kwamba yuko Mbinguni na hahitaji tena sala zetu.  Lakini mojawapo ya zawadi kuu zaidi tunazoweza kuwapa waliotangulia mbele yetu ni sala zetu.  Ni kweli kwamba kila mtu anayekufa katika hali ya neema…

Tafakari 147: Huruma kupitia Matendo, Maneno na Sala

Je, unataka kuwa chombo cha Huruma ya Mungu isiyopimika?  Ikiwa ndivyo, unafanya hivyo kwa matendo yako, maneno yako na sala zako.  Kwanza, lazima uwe macho daima kutafuta fursa za kuonyesha Huruma kwa matendo yako.  Mara nyingi sana, tunapopewa fursa (kama vile kumsamehe mwingine), tunageukia…

Tafakari 137: Nguvu katika Msalaba

Unaposali, je, wakati mwingine huketi na kuukazia macho msalaba wenye sanamu ya Yesu?  Kwa mtazamo wa mtu wa nje, msalaba huo ni jambo la kutatanisha.  Kwa nini tuinulie juu na kuheshimu tukio la kutisha namna hiyo?  Huenda mwanzoni mauaji ya kikatili ya Mwana wa Mungu yasiwe jambo linalotuvutia.  Hata hivyo…

Tafakari ya 131: Kazi Kubwa ya Sadaka Ndogo

Je, ni bora kufanya kazi kubwa au kutoa sadaka ndogo?  Ni rahisi kuhitimisha kwamba kazi fulani kubwa inayofanywa kwa ajili ya Mungu ni bora zaidi kuliko sadaka yoyote ndogo.  Lakini je, ni hivyo kweli?  Yote hayo yanategemea Mapenzi ya Mungu.  Wakati mwingine tunajitwika “kazi kubwa” fulani kwa ajili ya Mungu, lakini, mwishowe, si sehemu ya mpango Wake.  Kazi…

Tafakari ya 125: Nafsi Inayojitoa Sadaka

Je, unajua kwamba Bwana wetu huwachagua watu fulani kwa ajili ya utume maalumu wa kuteseka?  Yeye huwachagua watu fulani, ambao ni wachache, ili wafanane Naye kwa ukamilifu zaidi katika mateso aliyoyapata hapa duniani bila kuwa na hatia.  Nafsi hizi takatifu huteseka kwa njia nyingi na mbalimbali.  Wao ni mwendelezo wa…

Tafakari ya 113: Sadaka kwa Baba wa Milele

Sala kuu kuliko zote tunayoweza kusali ni “sala ya kujitoa sadaka.” Sala ya kujitoa sadaka ni dhabihu inayotolewa kwa Baba katika muungano na Dhabihu Moja ya Kristo Msalabani. Hatujitoi sisi wenyewe kwa nguvu zetu wenyewe. Tunajitoa katika muungano na Kristo Yesu. Hasa…

Tafakari 85: Kujikana kwa Ndani

Mojawapo ya zawadi kuu tunazoweza kumpa Bwana wetu wa Kimungu ni ukaidi wetu wa kushikilia matakwa yetu wenyewe.  Mara nyingi tunataka kile tunachokitaka, wakati tunapokitaka.  Utashi wetu unaweza kuwa mgumu na wenye ukaidi, na hali hii inaweza kutawala kwa urahisi nafsi yetu yote.  Kutokana na mwelekeo huu wa dhambi wa kushikilia matakwa yetu wenyewe, jambo moja…

Tafakari ya 77: Bwana Anajua Mambo Yote

Ni hakika kabisa kwamba Bwana wetu aliye Mungu anajua mambo yote.  Anajua kila wazo tulilo nalo na kila hitaji letu kwa kina zaidi kuliko tutakavyoweza kufahamu kamwe.  Nyakati fulani, tunapoanza kutambua ujuzi Wake mkamilifu, tunaweza kutarajia atimize mahitaji yetu yote hata kama…

Tafakari ya 62: Sadaka Ndogo za Maisha

Je, sadaka ndogo zina umuhimu?  Wakati mwingine tunaweza kufikiri kwamba tunapaswa kujaribu kufanya mambo makubwa.  Wengine wanaweza kuwa na mawazo ya makuu na kuota kutimiza mambo makubwa ya ajabu.  Lakini vipi kuhusu sadaka ndogo tunazotoa kila siku, tukirudia mambo yaleyale?  Sadaka kama vile kufanya usafi…

Tafakari ya 59: “Ee Damu na Maji…”

Baada ya kifo cha Yesu, mmoja wa askari alimwendea na akaamriwa kuhakikisha kwamba alikuwa amekufa.  Basi askari huyo aliuchoma mwili Wake wa thamani kwa mkuki, na mara damu na maji vikabubujika kutoka katika Moyo Wake uliojeruhiwa.  Jambo hili limetafakariwa kwa sala…