Kiswahili

Tafakari ya 42: Kutendewa Isivyo Haki Kunakotolewa kama Fidia ya Dhambi

Mara nyingi maishani tunatendewa isivyo haki.  Kwa hiyo, msukumo wetu wa kwanza ni kupambana na wanaotutendea hivyo, kujitetea na kuhakikisha kwamba haki inatendeka.  Lakini je, hivyo ndivyo Yesu alivyofanya?  La, alinyamaza na kukubali dhuluma zote kama sadaka ya kufidia dhambi zetu.  Alikuwa yule…

Tafakari 35: Kutambua Mateso ya Bwana

Je, unaelewa Mateso ya Bwana wetu?  Je, unayahisi mateso Yake nafsini mwako?  Mwanzoni, huenda hili likaonekana kuwa jambo lisilotamanika.  Lakini kutambua maumivu na Mateso ya Bwana wetu ni neema kubwa.  Tunapotambua mateso Yake, hatuna budi kuyakabili na kuyakumbatia kana kwamba ni yetu wenyewe.  Sisi…

Tafakari 365: Malkia wa Huruma

Tafakari hii ya mwisho imewekwa wakfu kwa Malkia wa Huruma, Mama wa Mungu Mwenye Utukufu Mkuu Sana.  Yeye, kuliko mwingine yeyote, alikuwa na anaendelea kuwa chombo kamilifu cha Huruma ya Mungu.  Aliileta Huruma yenyewe katika ulimwengu huu kwa jibu lake la “Na iwe,” yaani “Ndiyo,” wakati wa Kupashwa Habari.  Yeye…

Tafakari 362: Mioyo Miwili ya Huruma

Moyo wa Yesu ni Huruma tupu.  Ni chemchemi ya neema inayomiminika juu ya ulimwengu.  Hili linafariji, lakini kuna moyo mwingine ambao pia lazima uwe chemchemi ya Huruma, nao ni wako.  Lazima uzame sana katika Huruma ya Bwana kiasi kwamba moyo wako…

Tafakari 361: Sadaka na Sala

Ingawa huenda ikawa vigumu kuelewa na kuamini jambo hili, sadaka ya ndani iliyounganishwa na sala safi huleta manufaa makubwa ajabu kwa utangazaji wa Injili ulimwenguni kote.  Kwa kweli, kama wamisionari wasingekuwa na nguvu za watu watakatifu waliotoa kila siku sadaka za ndani…

Tafakari 348: Mungu Hutimiza Anayoyafunua

Inashangaza kuyatafakari mambo mawili ya hakika kwa pamoja.  Kwanza, tafakari jinsi Mtakatifu Faustina alivyomsikia Yesu akimwambia mara kwa mara kwamba alitaka Sikukuu ya Huruma ya Mungu itangazwe rasmi na kuadhimishwa katika Jumapili ya Pili ya Pasaka kila mwaka.  Je, mtawa huyu wa kike, mnyenyekevu aliyeishi maisha ya kujitenga monasterini, angewezaje kutimiza jukumu kama hilo…