Kiswahili

Tafakari ya 295: Kumbatio la Mtoto Yesu

Inafaa sana kutafakari kwa sala kuhusu kukumbatiwa katika mikono mitakatifu ya Mungu wetu.  Kuuelewa upendo wenye huruma wa Baba wa Mbinguni kupitia kumbatio takatifu la upendo kunatufunulia jinsi anavyotujali kama Baba.  Kukimbilia mikononi mwa Yesu kunaifungua mioyo yetu kwa upendo Wake wenye huruma.  Lakini taswira moja…

Tafakari ya 289: Shauku kwa Roho za Watu

Unapoitazama shauku iliyo moyoni mwako, ni nini kinachojitokeza zaidi?  Bila shaka kuna mambo mengi yanayokuvutia.  Thawabu na raha nyingi za kidunia zinaweza kwa urahisi kutawala matamanio yako.  Hamu ya raha za mwili, fedha na mafanikio ya kidunia ni miongoni mwa shauku zenye nguvu zaidi kwa…

Tafakari 288: Ukimya Unapokabiliwa na Dhihaka

Ukipewa zawadi tukufu ya imani thabiti, wengi wataiona na kuifurahia. Lakini inaweza kuwa sababu ya baadhi ya watu kuona wivu. Hili ni jambo la kusikitisha na lenye kuumiza. Ujue kwamba wivu wa mwingine hausababishwi na wewe wala na imani yako, bali unasababishwa na dhambi yake. Kwa hiyo, ukikabiliwa…

Tafakari 286: Unyenyekevu, Usafi na Upendo kwa Mungu

Ni nini kinachopendwa zaidi na moyo wa Mama yetu Mbarikiwa? Ikiwa angekutokea na kukuonyesha kile anachokutakia zaidi, kingekuwa nini? Huenda kungekuwa na hitaji fulani maalumu katika maisha yako ambalo Mungu amemjulisha, lakini pamoja na hilo…

Tafakari 284: Kuishi katika Wakati wa Sasa

Jaribu moja la kawaida ambalo wengi hukabili ni kuishi katika yaliyopita au katika yajayo, na kushindwa kuishi katika wakati wa sasa. Unaishi katika yaliyopita unapoendelea kutawaliwa na matukio, dhambi, maumivu, na mambo mengine ya zamani. Yaliyopita…

Tafakari 283: Kuishinda Dhambi

Ujumbe wa Huruma ya Mungu ni rahisi sana kiasi kwamba tunaweza kuukosa kwa urahisi, hata baada ya kutafakari kurasa nyingi za kitabu hiki au Shajara ya Mtakatifu Faustina.  Ukweli rahisi ambao ujumbe wa Huruma ya Mungu unapaswa kuwasilisha ni kwamba hatupaswi kuwa na hofu yoyote ile ya kukiri dhambi zetu…

Tafakari 281: Mapenzi ya Mungu Yasiyobadilika

Nyakati fulani, tunapompenda Mungu kwa upendo wa kina, tunaweza kujikuta tukisukumwa sana kufanya mambo makubwa kwa ajili Yake. Hata hivyo, licha ya hamu yetu na azimio letu thabiti, inaweza kuonekana kana kwamba Mungu haruhusu kazi yetu kusonga mbele. Huenda hii ni kwa sababu Bwana…

Tafakari ya 280: Kumpuuza Mungu

Je, unampuuza Mungu?  Ni rahisi mno kufanya hivyo na, kwa hiyo, hutokea mara nyingi sana.  Mara nyingi sana, Mungu hupuuzwa baada ya kupokea Komunyo Takatifu.  Watu wengi huzoea kusogea mbele ili kumpokea, nao hufanya hivyo huku mawazo yao yakitawanyika sana na bila kuuzingatia vya kutosha utakatifu wa…

Tafakari ya 279: Usadikisho Wako wa Ndani

Lazima ujitahidi kumsikia Mungu akisema nawe kwa njia ya usadikisho wa ndani katika nafsi yako.  Nyakati fulani unaweza kuhisi kwamba Sauti ya Mungu ni kubwa na wazi, na nyakati nyingine inaweza kuonekana hafifu na ya kutatanisha.  Kuna mambo mengi yanayoweza kushindana na Sauti ya Mungu…