Kiswahili

Tafakari ya 191: Nafsi Inayopenda Kuzungumza Sana

Hamu iliyopitiliza ya kuzungumza ni hatari halisi kwa maisha ya ndani ya ushirika na Mungu.  La, kuzungumza si dhambi, na mara nyingi ni tendo la Huruma kwa mwingine.  Lakini kuna nyakati ambapo kuzungumza kupita kiasi huwa kizuizi kwa Huruma ya Mungu.  Kuzungumza, kwenyewe tu, si…

Tafakari ya 190: Uumbaji Wote Unampa Mungu Utukufu

Vitu vyote vimeumbwa kwa lengo moja la mwisho: kuusifu na kuutukuza Utatu Mtakatifu.  Tumeumbwa kwa lengo hili tu, si kwa lengo kubwa zaidi, dogo zaidi, wala jingine lolote.  Sisi wanadamu tumeitwa kumpa Mungu sifa na utukufu wa pekee kwa kumwabudu kupitia maisha…

Tafakari ya 189: Kushinda Hofu

Hofu hutokana na sababu mbalimbali.  Kutambua tishio lililo mbele yako husababisha hofu ya ghafla kama njia fulani ya kujilinda.  Kwa kweli, jambo hili linaweza kuokoa maisha yako ikiwa, kwa mfano, tishio hilo ni gari linalogeuka kwa ghafla na kuingia katika njia yako.  Hofu ya ghafla hukusukuma kuchukua…

Tafakari 188: Matakwa ya Bwana

Bwana akikuomba ufanye jambo fulani, je, una chaguo?  Unalo kwa kuwa unaweza kusema “Hapana.”  Na kufanya hivyo ni dhambi.  Lakini ikiwa umechagua kumfuata Kristo na lengo lako ni Mbingu, basi ni sahihi kusema kwamba tuna wajibu wa kufanya chochote Bwana anachotuomba.  Yake…

Tafakari 187: Upinde wa Mvua baada ya Dhoruba

Inastaajabisha jinsi uumbaji wenyewe unavyotangaza utukufu wa Mungu na kutufundisha mambo ya imani. Chukua mfano wa upinde wa mvua. Unang’aa na unapendeza, una rangi nyingi na unatia mshangao. Kila mtu hufurahi anapoona upinde wa mvua. Lakini upinde wa mvua usingekuwapo bila mvua au dhoruba. Ndivyo yalivyo maisha. Sisi…

Tafakari 186: Kupenywa na Mungu

Je, roho yako “imepenywa” na Mungu? Je, Yeye “anakujaza kabisa”? Je, unajiruhusu “kuyeyuka” katika uungu Wake na “kuzungukwa” na Huruma Yake? Kuna maneno mengi sana tunayoweza kutumia kueleza uhusiano wetu na Mungu. Ingawa yote yanasaidia kueleza Mungu ni nani na ni…

Tafakari 185:  Ukarimu kwa Rasilimali Zisizo na Kikomo

Kama ungejua kwamba kuna njaa kali katika nchi ya mbali, na pia ungebarikiwa kuwa na rasilimali zisizo na kikomo za kukabiliana na njaa hiyo, kwa nini ungewanyima wenye uhitaji zawadi hii?  Tunatumaini kwamba usingefanya hivyo.  Tunatumaini kwamba ungetambua wajibu wako na kufanya yale yaliyohitajika…

Tafakari 184: Huruma katika Huduma ya Mapadre

La, mapadre si wakamilifu.  Wanatenda dhambi siku baada ya siku.  Wanahitaji daima kutubu na kuongoka katika maisha yao ya kila siku, kama wanadamu wengine wote.  Lakini wao ni mapadre.  Na kwa sababu ya upadrisho wao mtakatifu, Bwana huzungumza kupitia kwao kwa njia iliyo wazi…

Tafakari ya 183: Kuzingatia Thamani ya Mateso

Tunapoteseka, tunatafuta njia ya kutoka katika mateso.  Tunatafuta nafuu.  Lakini tukiwa Mbinguni, tutaweza kutazama nyuma na kuona nguvu kuu ya mateso yaliyochaguliwa na kukumbatiwa kwa hiari.  Si kwamba mateso ni mema yenyewe; bali ni kwamba mateso yamekombolewa na kupewa…

Tafakari 182: Hekima ya Kupenya Siri za Kiburi

Kiburi kinaweza kututawala kabisa.  Hilo linapotokea, tunachofikiria tu ni sisi wenyewe na uchungu wetu.  Labda unaelewa hali hii kutokana na uzoefu wako.  Huenda umejeruhiwa moyoni, nawe unakaa ukinuna kwa sababu ya jeraha hilo.  Linatia uchungu moyoni mwako, nawe unatafuta kuliponya.  Lakini…