Kiswahili

Tafakari 137: Nguvu katika Msalaba

Unaposali, je, wakati mwingine huketi na kuukazia macho msalaba wenye sanamu ya Yesu?  Kwa mtazamo wa mtu wa nje, msalaba huo ni jambo la kutatanisha.  Kwa nini tuinulie juu na kuheshimu tukio la kutisha namna hiyo?  Huenda mwanzoni mauaji ya kikatili ya Mwana wa Mungu yasiwe jambo linalotuvutia.  Hata hivyo…

Tafakari ya 133: Kutenda kwa Kujitegemea

Hatuwezi kufanya jambo lolote jema kwa kujitegemea wenyewe.  Huu ni ukweli.  Tunachoweza kufanya kwa kujitegemea wenyewe ni kutenda dhambi tu.  Kwa kweli, njia pekee ya kumpendeza Mungu na kumfanyia mambo mema ni kumtegemea kwa kila kitu.  Lazima tuwe na uhusiano wa kumtegemea Mungu kikamilifu katika mambo yote…

Tafakari ya 130: Kuwarekebisha Wengine kwa Upendo

Karibu hakuna shaka kwamba kila mmoja wetu atakutana, mara kwa mara, na dhambi ya mtu mwingine.  Inaweza kuwa katika maneno yake, matendo yake au kuacha kufanya yale anayopaswa kufanya.  Dhambi huumiza na inahitaji marekebisho.  Mara nyingi sana, wengine wanapotukosea, tunaelekea kukasirika.  Lakini…

Tafakari 126: Hofu ya Kimwana – Hofu Njema

Je, una hofu maishani mwako?  Ni muhimu kujua kwamba hofu fulani haifai kabisa, kwani hutokana na aina fulani ya kiburi, ilhali aina nyingine ya hofu ni njema sana, kwani hutokana na upendo wako wa kina kwa Mungu.  “Hofu takatifu” ni hofu ya kimwana, yaani hofu ya mtoto wa Mungu.  Hofu hii…

Tafakari 119: Kujikana kwa Ndani na kwa Nje

Kujikana ni zoea la kukataa kufuata matakwa yako ili uzidi kujifungua kutoka katika kushikamana na mambo ya ulimwengu huu yanayopita.  Tunapaswa kujitahidi kuacha kushikamana na kila kitu isipokuwa Mungu na Mapenzi Yake matakatifu.  Si kwamba kila tunachokipenda au kukitamani ni kibaya, lakini ikiwa tunataka utakatifu wa kweli, hamu yetu…

Tafakari 117: Eneo la Faragha la Moyo Wako

Baadhi ya masista na wamonaki huishi maisha ya kujitenga ndani ya mipaka ya eneo la faragha.  Hakuna anayeruhusiwa kuingia katika eneo hilo bila sababu ya msingi, isipokuwa awe mwanajumuiya hiyo ya imani. Wengine wanaweza kuingia tu kwa ruhusa ya mkuu wa jumuiya.  Huenda ikawa…

Tafakari ya 115: Mapenzi ya Mungu Yatakuhifadhi Salama

Mapenzi ya Mungu ni zaidi sana ya mpango wa siku zijazo ambao Mungu amekuandalia.  Ni zaidi ya matumaini na ndoto Zake kwa ajili yako.  Mapenzi Yake ndiyo njia yako ya kuelekea utakatifu, nayo ni chemchemi ya faraja na furaha kuu.  Mapenzi Yake yana namna ya kutenda na pia ya kutotenda (kuruhusu).  Ni…

Tafakari 114: Kutofungamana na Ulimwengu

“Ulimwengu” unatajwa mara nyingi katika Maandiko Matakatifu, hasa na Yesu Mwenyewe. Alisema kwamba ulimwengu utakuchukia na hautakuelewa. Kwa kweli, ulimwengu utakutesa. Hili linaweza kuwa sababu ya hofu na dhiki kwa baadhi ya watu. Linasababisha hali hizi ndani…

Tafakari ya 111: Uongo wa Mwovu

Ibilisi atatujaribu kwa njia nyingi.  Njia moja ya kawaida ambayo ibilisi hupenda kutumia kutushambulia ni kutukumbusha dhambi zetu, kutia ndani zile tulizokwisha kuungama.  Hupenda kujaribu kutushawishi kwamba tuko katika njia potovu, kwamba hatumpendezi Mungu, kwamba sisi ni waongo na wenye dhambi.  Na…

Tafakari ya 110: Miale ya Huruma

Huruma ya Moyo wa Yesu inang’aa kwa uangavu mkuu. Hii ndiyo iliyokuwa picha ya Huruma ya Mungu ambayo Mtakatifu Faustina aliiona. Moyo ulio wazi wa Bwana wetu ulifurika, ukimimina mwanga na neema juu ya ulimwengu. Yesu anataka kuendelea kuuangazia ulimwengu…