Kiswahili

Tafakari 275: Utukufu wa Siku Zisizo na Msisimko

Kwa mtazamo wa kwanza, huenda maneno “kutokuwa na msisimko” na “utukufu” yasionekane kuendana isipokuwa yanapotumiwa kuonyesha tofauti.  Lakini maneno haya mawili yameoanishwa katika Fikra za Mungu.  “Yameoanishwa” kwa maana kwamba tunaweza kumtukuza Mungu na kupata utakatifu kupitia majukumu yetu ya kila siku yasiyo na msisimko.  Ingawa…

Tafakari 274: Kufanya Upya Nadhiri Zako

Ni desturi ya kawaida kwa walio katika ndoa kufanya upya nadhiri zao mara kwa mara, hasa katika maadhimisho muhimu ya ndoa zao.  Mapadre na watawa pia hufanya upya nadhiri na ahadi zao.  Desturi hii ni njema na takatifu kwa kuwa tunapaswa daima kufanya upya…

Tafakari 273: Bila Mafungamano ya Kidunia, Upendo kwa Mungu Pekee

Kilele cha uhusiano wetu na Mungu kinahusisha kuondolewa kila fungamano jingine la kidunia ili kusiwe na kitu kinachotuzuia kumkimbilia Mungu kwa shauku kubwa na nia thabiti.  Lazima tuwekwe huru kutoka katika kila kifungo cha maisha haya ili tushikamane na Mungu pekee na yale Yake matakatifu…

Tafakari 272: Kudhihirika kwa Moyo kwa Nje

Hakuna anayeweza kuuona moyo wako isipokuwa wewe na Mungu.  Mungu anajua kikamilifu kila undani wa maisha yako ya ndani; wewe huoni kikamilifu undani wa maisha yako ya ndani.  Hata hivyo, ni muhimu kuendelea kutambua zaidi na zaidi hali halisi ya maisha yako ya ndani.  Tazama…

Tafakari ya 271: Kutazama Zaidi ya Vikwazo vya Maisha

Mwelekeo na kishawishi kimoja kilicho cha kawaida sana ambacho watu wengi hupambana nacho ni kukazia fikira mateso, fedheha na maoni potofu ya wengine.  Tunapopatwa na mojawapo au zaidi ya mizigo hii, tunaweza kushawishika kuifanya kuwa kiini cha maisha yetu.  Kwa mfano…

Tafakari 270: Vipengele vya Mapenzi ya Mungu

Je, uko tayari kuyakubali Mapenzi ya Mungu katika maisha yako?  Ikiwa ndivyo, lazima uwe tayari kupokea kila kipengele chake.  Mapenzi ya Mungu si wazo la jumla lenye ukuu wa kuvutia tu.  Kuyachagua Mapenzi Yake si kusema tu kwamba unachagua kumfuata kwa ujumla.  Badala yake, kuyachagua Mapenzi Yake…

Tafakari 269: Kutazama Mambo Mawili: Huruma na Unyonge

Kama ungeweza kuchagua mambo mawili ya kuyatazama kwa tafakari, yangekuwa yapi?  Kwa hakika, mambo mawili muhimu zaidi ya kuyatazama ni Huruma ya Mungu na unyonge wako mwenyewe.  Yaelekea unaelewa mara moja kwamba Huruma ya Mungu ingekuwa mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuyatazama…

Tafakari 267: Haki au Huruma?

Inafaa kuzungumza kuhusu Haki ya Mungu na pia Huruma Yake.  Havipingani.  Haki Yake itatekelezwa kwa wale wanaokataa kutubu, kama ilivyotekelezwa kwa malaika waliokataa kumtumikia Mungu.  Lakini, kwa sasa, inafaa zaidi kusema kwamba Mungu ni Mwenye Huruma.  Kwa kweli…

Tafakari 266: Kuvunjika Moyo Mbele ya Utakatifu

Je, unataka kuwa mtakatifu? Tunatumaini jibu ni “Ndiyo.” Lakini vipi kuhusu swali hili: Je, unafikiri unaweza kuwa mtakatifu? Huenda ikawa vigumu zaidi kujibu swali hili. Ni rahisi kuota kuhusu utakatifu na kutamani…

Tafakari 265: Hatari na Baraka ya Mihemko

Mungu alituumba tukiwa na mihemko.  Mihemko hii inaweza kuwa baraka kubwa katika safari yetu ya Kikristo, au inaweza kuwa mitego mikubwa.  Yote hutegemea kile kinachotawala kila mhemko.  Kwa mfano, mihemko ya hasira inaweza kutumiwa kwa wema au kwa uovu.  Hasira inapotutawala na chanzo cha hasira hiyo…