Kiswahili

Tafakari 221: Kujitukuza

Wakati mwingine, wale walio “watu wa dini” sana huzungumzia mambo mengi “ya dini”.  Hutumia lugha ya uchaji na kuzungumzia mambo matakatifu.  Lakini hatimaye, huenda yote wanayosema na kufanya kwa kweli yanasemwa na kufanywa ili kujitukuza mbele ya wengine.  Hii ndiyo changamoto…

Tafakari ya 210: Matendo Mema katika Mwanga wa Upendo wa Mungu

Je, unafanya kazi kwa bidii?  Je, unajitahidi kuwa mwema?  Je, unataka kuleta mabadiliko yenye manufaa?  Hakika ni vema kujitahidi kuwa mwema.  Lakini tunapofanya hivyo, hatupaswi kamwe kufikiri kwamba “wema” wetu ni mwema kweli machoni pa Mungu, isipokuwa Upendo wa Mungu ndio umekuwa chanzo…

Tafakari 184: Huruma katika Huduma ya Mapadre

La, mapadre si wakamilifu.  Wanatenda dhambi siku baada ya siku.  Wanahitaji daima kutubu na kuongoka katika maisha yao ya kila siku, kama wanadamu wengine wote.  Lakini wao ni mapadre.  Na kwa sababu ya upadrisho wao mtakatifu, Bwana huzungumza kupitia kwao kwa njia iliyo wazi…

Tafakari 178: Utakatifu Haupatikani Kamwe kwa Nguvu Zetu Pekee

Je, unatamani kuishi maisha matakatifu?  Ikiwa ndivyo, huwezi kufanya hivyo kwa nguvu zako pekee.  Unahitaji msaada wa mtu mwingine, na hata wa watu wengine wengi.  Bwana ametupatia njia nyingi za kuongozwa kwa upendo na wengine.  Baadhi wamejaliwa kuwa na kiongozi wa kiroho wa miaka mingi…

Tafakari 176:  Kupambana na Dhambi ya Ulimwengu

Mungu anapoutazama ulimwengu, anaona nini?  Bila shaka anaona uzuri wa uumbaji Wake, mpangilio mkamilifu wa kusudi Lake na uwepo wa wana na binti Zake.  Lakini pia anaona ubaya wa kutisha wa wingi wa dhambi.  Hata dhambi ndogo kabisa…

Tafakari ya 169: Utulivu Mbele ya Mfalme

Kukutana na mtu mwenye mamlaka makubwa kunaweza kuleta msisimko.  Kwa mfano, kukutana na rais wa kampuni unayotamani kufanya kazi ndani yake, au kukutana na mtu maarufu kwa mara ya kwanza, au kukutana na askofu au Baba Mtakatifu, yote hayo yanaweza kuleta msisimko fulani.  Lakini…

Tafakari 163: Kumtukuza Mungu katika “Unyonge” Wako

Je, unaona unyonge wa roho yako mwenyewe?  Huenda wengine wakakwazika kwa swali kama hili.  Lakini kama tungeielewa Huruma ya Mungu, na kutambua kwamba ni “unyonge” wetu unaomwezesha Yeye kutukuzwa zaidi, tusingeikwepa fikra kama hiyo.  Wengi…

Tafakari 160: Huruma katika Kitubio

Je, umegundua furaha kubwa ya kwenda kuungama? Baadhi ya watu hawaioni Sakramenti ya Kitubio kuwa chanzo cha furaha kubwa. Badala yake, wanaiona kuwa jambo lenye maumivu na linalowaaibisha. Lakini huenda wengine wanahitaji aibu inayotokana na kuungama kwa unyofu…

Tafakari ya 157: Kufanya Maamuzi ya Kimaadili

Je, wakati mwingine unapata shida kufanya uamuzi ulio sahihi kimaadili? Hali hii hutokana na asili yetu ya kibinadamu iliyoanguka dhambini. Tunachanganyikiwa kwa urahisi maishani na tunaweza kushindwa kwa urahisi kufahamu Mawazo na Mapenzi ya Mungu. Basi ufanye nini? Jua kwamba dhamiri yako ni patakatifu ambapo…

Tafakari ya 154: Kuabudu kwa Ukimya na Unyenyekevu

Wazia Mama yetu Mbarikiwa katika hali duni wakati wa Kuzaliwa kwa Yesu.  Wakati huo hakuwa na makao mengine isipokuwa mahali hapa walipokusanyika wanyama.  Hata hivyo, katika utulivu wa usiku ule mtakatifu, alijisikia kuwa nyumbani alipomtazama Mtoto wake kwa ibada ya kuabudu na upendo wa kina kabisa.  Yeye…