Kiswahili

Tafakari ya 107: Kuifunua Nafsi Yako katika Ungamo

Mungu anatutumia mapadri Wake kuwa wawakilishi Wake.  Ingawa mapadri si wakamilifu, bado wao ni wawakilishi wa Mungu.  Hili ni kweli hasa katika Sakramenti ya Upatanisho.  Ni muhimu tuikaribie Sakramenti hiyo…

Tafakari ya 102: Mungu Huwatumia Walio Dhaifu

Kama ungekuwa Mungu, na ungekuwa na kazi fulani tukufu ambayo ungetaka itimizwe, ungemchagua nani?  Mtu mwenye vipawa vilivyo wazi?  Au mtu aliye dhaifu, mnyenyekevu na anayeonekana kuwa na vipawa vichache sana vya asili?  Jambo la kushangaza ni kwamba, mara nyingi Mungu huwachagua walio dhaifu kwa…

Tafakari 99: Mjeledi wa Dhambi

Kwa nini Yesu aliteseka namna ile?  Kwa nini alipigwa mijeledi kwa ukali kiasi kile?  Kwa nini kifo Chake kilikuwa na maumivu makali kiasi kile?  Kwa sababu dhambi ina matokeo na ni chanzo cha maumivu makubwa.  Lakini Yesu kuyakubali mateso kwa hiari na bila dhambi kuliyageuza…

Tafakari ya 98: Kuwa Chombo

Mungu anapotuita kutimiza utume fulani, ni nani anayetenda kazi?  Mungu au sisi?  Ukweli ni kwamba sote tunatenda kazi: Mungu ndiye chanzo nasi ni chombo.  Tunajitahidi kwa hiari yetu, lakini ni Mungu anayeangaza kupitia sisi.  Kama vile dirisha linavyoweza kuwa chanzo cha mwanga…

Tafakari ya 71: Udogo Wetu na Hali Yetu ya Kutokuwa Kitu

Ni neema kutoka kwa Mungu kujiona jinsi tulivyo.  Na tutaona nini tukijiona kwa namna hii?  Tutaona unyonge wetu na hali yetu ya kutokuwa kitu.  Mwanzoni, huenda jambo hili lisituvutie sana.  Huenda hata likaonekana kuwa kinyume na hadhi tuliyo nayo katika Kristo.  Lakini hapo ndipo ufunguo ulipo.  Yetu…

Tafakari ya 63: Unazungumzaje na Wengine?

Tunapozungumza na wengine, upendo na Huruma ya Mungu lazima vitiririke kutoka midomoni mwetu. Lakini kwa namna gani? Usemi wetu unapaswa kuwaje? Njia mojawapo ya kuchunguza usemi wetu kwa wengine ni kuutazama kwa kuzingatia jinsi tunavyopaswa kuzungumza na Mungu. Tunapozungumza na Mungu tunapaswa kusema kwa uaminifu…

Tafakari ya 37: Unyenyekevu, Usahili na Unyofu

Kuna maneno matatu ya kutafakari leo: unyenyekevu, usahili na unyofu. Watu wanyenyekevu humwona na kumjua Mungu kwa sababu hawajitegemei wenyewe wanapokuwa na uhitaji. Wanatambua kwamba Mungu ndiye kila kitu na kwamba, bila Yeye, wao si kitu. Watu wenye usahili hawanaswi…

Tafakari ya 32: Huruma ya Kusamehe

Katika maisha yako yote, utaumizwa na dhambi za wengine. Hili haliepukiki. Swali la msingi la kutafakari ni jinsi unavyoyashughulikia maumivu haya. Je, utayang’ang’ania na kuendelea kuyawazia kwa uchungu? Au utasamehe? Lakini kusamehe hakutoshi. Lazima uiruhusu Huruma ya Mungu iingie ndani ya roho yako kiasi kwamba…

Tafakari ya 31: Asili ya Mungu Isiyoweza Kufahamika Kikamilifu

Hatuwezi kumjua Mungu katika dhati Yake.  Yeye anapita ufahamu wetu na hawezi kufahamika kikamilifu.  Lakini tunaweza kumjua Mungu kwa kuona matendo Yake katika maisha yetu na ulimwenguni.  Tazama sifa Zake.  Tazama kazi Zake.  Tazama yale aliyoyatenda katika maisha yako na katika…

Tafakari ya 30: Kumtii Mungu

Utii ni ufunguo mmoja wa utakatifu.  Adamu na Hawa walipoteza neema kwa kutotii, nasi tunarudishiwa neema kwa kutii.  Utii unaweza kuwa mgumu na unahitaji uamuzi wa dhati kutoka ndani ya moyo.  Tafuta fursa za kumtii Yesu, hasa wakati wewe…