Kiswahili

Tafakari 318: Kutojali na Kusahau

Kama ungekuwa katika ndoa na mara kwa mara ukawa humjali mwenzi wako, hilo lingekuwa tatizo.  Kutojali maana yake ni kutokuwa na moyo wa kujali kwa dhati mema ya mwingine.  Kusahau ni dalili ya kutojali kwa kuwa mtu asipojali sana, ni rahisi kwake kusahau.  Kwa mfano…

Tafakari 298: Virusi vya Masengenyo Yasiyo na Maana

Mwelekeo mmoja wa kusikitisha katika asili yetu ya kibinadamu iliyoanguka ni “kumsengenya” mwingine.  Ni kama virusi kwa kuwa mtu mmoja anapoanza, huenea upesi kwa wengine.  Muda si muda, watu wengi wanaweza kuwa wanaeneza uvumi na masengenyo yasiyo na msingi katika ukweli, au ukweli unaosemwa bila upendo.  Hili…

Tafakari ya 296: Upendo wa Mzazi

Mwazie mzazi anayempenda mtoto kwa upendo unaowaka moyoni.  Anajitolea kwa kila namna kumtunza mtoto wake na kuhakikisha ustawi wake.  Upendo wake ni thabiti na hautenguki tangu mtoto anapozaliwa hadi anapokuwa mtu mzima.  Sasa wazia uchungu moyoni mwa mzazi huyu ikiwa wakati fulani mtoto wake anaondoka…

Tafakari 284: Kuishi katika Wakati wa Sasa

Jaribu moja la kawaida ambalo wengi hukabili ni kuishi katika yaliyopita au katika yajayo, na kushindwa kuishi katika wakati wa sasa. Unaishi katika yaliyopita unapoendelea kutawaliwa na matukio, dhambi, maumivu, na mambo mengine ya zamani. Yaliyopita…

Tafakari ya 199: Umoja na Yesu ni Umoja na Wengine

Kanisa lina utukufu kwa sababu nyingi. Mojawapo ya mambo yenye utukufu katika Kanisa ni umoja uliomo ndani yake. Ni kweli kwamba nyakati fulani kuna migawanyiko mingi ndani yake, maumivu na machafuko ya kila aina. Lakini haya si sifa za Kanisa. Haya ni matokeo ya dhambi…

Tafakari 182: Hekima ya Kupenya Siri za Kiburi

Kiburi kinaweza kututawala kabisa.  Hilo linapotokea, tunachofikiria tu ni sisi wenyewe na uchungu wetu.  Labda unaelewa hali hii kutokana na uzoefu wako.  Huenda umejeruhiwa moyoni, nawe unakaa ukinuna kwa sababu ya jeraha hilo.  Linatia uchungu moyoni mwako, nawe unatafuta kuliponya.  Lakini…

Tafakari 109: Mikono ya Mungu

Mtoto anapoogopa au kuumia, kwa kawaida hupata faraja mikononi mwa mzazi.  Hili ndilo jambo la kwanza ambalo mtoto anayelia hutafuta.  Ndivyo inavyopaswa kuwa kwetu pia.  Tunapokuwa na uhitaji, tunapaswa kukimbilia mikononi mwa Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Mwokozi wetu.  Tunapaswa…

Tafakari ya 66: Haki kwa Njia ya Huruma

Watu wengine, siku baada ya siku, wanakabiliwa na ukali na ukatili wa mtu mwingine.  Hili linaumiza sana.  Kwa sababu hiyo, wanaweza kuwa na hamu kubwa ya haki ili anayesababisha maumivu awajibishwe.  Lakini swali la msingi ni hili: Bwana ananiita nifanye nini?  Nita…

Tafakari ya 32: Huruma ya Kusamehe

Katika maisha yako yote, utaumizwa na dhambi za wengine. Hili haliepukiki. Swali la msingi la kutafakari ni jinsi unavyoyashughulikia maumivu haya. Je, utayang’ang’ania na kuendelea kuyawazia kwa uchungu? Au utasamehe? Lakini kusamehe hakutoshi. Lazima uiruhusu Huruma ya Mungu iingie ndani ya roho yako kiasi kwamba…