Kiswahili

Tafakari 267: Haki au Huruma?

Inafaa kuzungumza kuhusu Haki ya Mungu na pia Huruma Yake.  Havipingani.  Haki Yake itatekelezwa kwa wale wanaokataa kutubu, kama ilivyotekelezwa kwa malaika waliokataa kumtumikia Mungu.  Lakini, kwa sasa, inafaa zaidi kusema kwamba Mungu ni Mwenye Huruma.  Kwa kweli…

Tafakari ya 263: Mungu kama Nahodha Wako katika Dhoruba

Jiwazie ukiwa mtoto mdogo katika mashua ndogo katikati ya bahari. Dhoruba inaanza, wala huwezi kuona nchi kavu upande wowote. Mawimbi yanakurusha na kukugeuza, yakifunika omo la mashua kila yanapoipiga, nawe unajiuliza utawezaje kupona. Sasa jiwazie kwamba baba yako…

Tafakari 261: Yesu Aliyejificha Ndani ya Wengine

Fikiria kama Yesu angekujia akiwa maskini, mwenye njaa na baridi, na kukuomba umtunze.  Hali hii huenda ikakushtua na kukufanya ujiulize kama kweli mtu huyo ni Yesu.  Lakini ni Yesu.  Yesu hutujia kila siku katika mtu mwenye uhitaji.  Huenda…

Tafakari ya 248: Rasilimali Zisizo na Kikomo

Hebu fikiria kama ungepata chanzo cha rasilimali za asili zisizo na kikomo kwa kutengeneza mashine inayobadili kiasi kidogo tu cha oksijeni kuwa nishati isiyo na kikomo.  Ungehitaji tu kuwasha mashine uliyotengeneza, nayo ingezalisha nishati…

Tafakari 240: Utamu au Uchungu Maishani?

Unapendelea nini katika maisha yako?  Kuhisi utamu au uchungu kila siku?  Kwa maneno mengine, je, unatamani kufurahia mambo mengi ya maisha yako ya kila siku, au unatamani kwamba wajibu unaoutimiza kila siku ukuache na uchungu fulani ndani yako…

Tafakari ya 239: Muhuri wa Huruma

Kila mtakatifu mkuu ni kielelezo cha kipengele fulani cha wema wa Mungu.  Wengine wanaishi kwa kujitenga kwa namna ya pekee na utajiri wa kidunia, wengine wanawahudumia maskini kwa kujitoa bila kuyumba, wengine wanaishi maisha ya sala ya kina, wengine wanapata mafunuo ya kimafumbo, wengine wanaandika majuzuu ya…

Tafakari ya 232: Kuituliza Dhoruba

Kumbuka simulizi la Yesu akiituliza dhoruba (Mathayo 8:23-27).  Tendo hili la kimiujiza lilifanywa kama ishara ya kinabii ya Yeye kukuletea amani wakati wa changamoto mahususi unazokabiliana nazo maishani…

Tafakari ya 211: Karibu na Mama wa Mungu

Upendo wa mama unaweza kuelezwa kuwa “wenye nguvu” kwa maana kwamba angekuwa tayari kutoa uhai wake ili kuwalinda watoto wake.  Msukumo wa asili wa kimama huamka wakati mtoto wake yuko hatarini, anaumia, au ana uhitaji, naye husahau kabisa ustawi wake mwenyewe ili kumlinda…

Tafakari ya 208: Mshale wa Kiroho wa Huruma

Kwa kawaida, mshale hujeruhi na kuua. Mishale imetumiwa katika historia yote kwa vita na kwa kuwinda. Lakini mshale wa kiroho wa Huruma ni tofauti sana. Kumbuka maneno ya nabii Simeoni aliyomwambia Mama yetu Mbarikiwa, “Na wewe mwenyewe upanga utakuchoma” (Luka 2:35). Na…

Tafakari ya 207: Kupata Faraja katika Moyo wa Kristo

Mara nyingi watoto hupata faraja kubwa wanapojibanza karibu na mzazi mwenye upendo na wororo.  Kuna uradhi mkubwa katika kukumbatiwa kwa nguvu na mikono hii yenye upendo.  Katika nyakati hizi, hofu na wasiwasi huondoka, na amani na kitulizo hurudi pale palipokuwa na dhiki.  Ndivyo inavyopaswa…