Kiswahili

Tafakari ya 149: Maongozi ya Ndani

Kuna fursa zisizohesabika kila upande wetu za kuwashirikisha wenye uhitaji Huruma ya Mungu. Lakini ni rahisi sana kuzikosa fursa hizi. Njia moja kuu ya kujiruhusu kuwa vyombo vya Huruma ya Mungu ni kujitahidi daima kuwa wasikivu…

Tafakari ya 143: Kutumaini, Kutumaini na Kutumaini Zaidi

Kila tafakari katika kitabu hiki inahitimishwa kwa sala, na kila sala inahitimishwa kwa sala hii: “Yesu, nakutumainia.”  Lakini je, kweli unamtumainia?  Kutumaini si tendo la mara moja tu.  Si jambo la kusema tu kwamba tunatumaini au hatutumaini.  Ni jambo ambalo lazima tulifanye kwa kina kinachozidi kukua daima.  Hakuna kikomo cha kina…

Tafakari ya 140: Kutoeleweka

Katika mahusiano yako na wengine, je, wakati mwingine unahisi kwamba hawaelewi unachomaanisha?  Huenda akawa mwanafamilia wa karibu, rafiki, mfanyakazi mwenzako, n.k.  Tatizo ni kwamba yaliyomo katika akili yako, moyo wako, utashi wako, nia yako, na mambo yote uliyopitia zamani ndiyo yanayoongoza namna unavyo…

Tafakari ya 136: Nguvu ya Moyo Wenye Shukrani

Kama ungechunguza maudhui ya maisha yako ya sala katika mwezi uliopita, ungeona nini?  Inatumainiwa kwamba kungekuwa na nyakati nyingi za kujikabidhi, maombezi, sifa na kuabudu.  Na inatumainiwa kwamba pia kulikuwa na nyakati nyingi ambapo sala yako ilikuwa ya kutoa shukrani za dhati kwa…

Tafakari 135: Kuzungumza na Yesu

Je, unazungumza na Yesu?  Hii ni namna ya sala inayozaa matunda mengi sana.  “Mazungumzo” na Mungu si namna ya juu kabisa ya sala, lakini ni namna ya sala ambayo mara nyingi tunahitaji kuanzia nayo.  Mazungumzo na Mungu huzaa matunda hasa tunapobeba mzigo fulani…

Tafakari ya 131: Kazi Kubwa ya Sadaka Ndogo

Je, ni bora kufanya kazi kubwa au kutoa sadaka ndogo?  Ni rahisi kuhitimisha kwamba kazi fulani kubwa inayofanywa kwa ajili ya Mungu ni bora zaidi kuliko sadaka yoyote ndogo.  Lakini je, ni hivyo kweli?  Yote hayo yanategemea Mapenzi ya Mungu.  Wakati mwingine tunajitwika “kazi kubwa” fulani kwa ajili ya Mungu, lakini, mwishowe, si sehemu ya mpango Wake.  Kazi…

Tafakari ya 129: Usiwe na Hofu

“Usiwe na hofu; uwe tu na imani” (Marko 5:36).  Maneno haya manne, “Usiwe na hofu,” yanasemwa mara zisizohesabika katika Maandiko Matakatifu.  Tunapaswa kuyazingatia.  Hofu inaweza kutufanya tushindwe kutenda na kutuongoza katika namna nyingi za kufikiri na kutenda kwa upumbavu.  Mtu…

Tafakari 128: Utamu wa Kukutana na Yesu

Je, umewahi kuonja utamu wa Yesu?  Yeye, pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, huja kwako katika vilindi vya siri vya nafsi yako.  Humo, katika mahali hapa pa siri, wanatamani kuwasiliana nawe.  Mawasiliano yao yanapita maneno na dhana.  Ni…

Tafakari 126: Hofu ya Kimwana – Hofu Njema

Je, una hofu maishani mwako?  Ni muhimu kujua kwamba hofu fulani haifai kabisa, kwani hutokana na aina fulani ya kiburi, ilhali aina nyingine ya hofu ni njema sana, kwani hutokana na upendo wako wa kina kwa Mungu.  “Hofu takatifu” ni hofu ya kimwana, yaani hofu ya mtoto wa Mungu.  Hofu hii…

Tafakari ya 122: Kama Ungeweza Kuchagua

Kama ungeweza kuchagua kati ya utajiri wote wa ulimwengu na uhusiano wa karibu na wenye upendo na Yesu, ungechagua nini? Usijibu haraka mno. Huenda tukajua kwamba kumchagua Yesu ndilo jibu sahihi, lakini je, ungemchagua? Fikiria mamlaka na “uhuru” wa kidunia ambao unge…