Kiswahili

Tafakari 356: Mapigo ya Moyo Wako

Unapokuwa na msisimko maishani mwako, moyo wako huanza kudunda kwa kasi zaidi.  Hili ni jambo la kawaida katika mwili.  Kwa sababu hiyo, ni vizuri kutafakari: je, moyo wako huwahi kudunda kwa ajili ya Mungu?  Je, unajiruhusu kujawa na kicho kitakatifu mbele ya uwepo wa Mungu?  Je…

Tafakari ya 354: Kuufumua Utando wa Dhambi

Mtu anapoanza kusema uongo na kuufanya kuwa mazoea, hatimaye atanaswa katika utando wa uongo.  Uongo mmoja huzaa mwingine, na muda si mrefu hajui jinsi ya kujinasua katika utando huo.  Hapo ndipo unapopaswa kumwonyesha huruma.  Ni rahisi sana kumtendea kwa ukali…

Tafakari ya 353: Wimbo wa Utukufu

Muziki ni ugunduzi na udhihirisho wa sheria za asili za uumbaji wa Mungu, ukitegemea mpangilio na mdundo uliomo katika muundo wake wa asili.  Muziki fulani hutumia mpangilio wa asili wa vitu kutukuza mambo ya kidunia.  Baadhi ya aina za muziki hata hudhihirisha dhambi na ukosefu wa mpangilio.  Lakini…

Tafakari ya 352: Adhabu na Hisia ya Hatia

Huenda isiwe jambo la kupendeza kutafakari adhabu ya Mungu.  Lakini lazima ieleweke kwamba adhabu Zake ni halisi na ni tendo la Huruma Yake tele.  Nafsi zinapomwacha Mungu na kuikataa Huruma Yake, jambo hili linaujeruhi sana Moyo Wake.  Kwa sababu hiyo, Mungu anakuwa…

Tafakari 351: Kumjua Mungu au Kuwa na Uzoefu Wake

Kumjua Mungu lazima kuwe lengo lako la daima. Kujifunza Maandiko Matakatifu, mafundisho ya Kanisa na maisha ya watakatifu kunasaidia katika jitihada hii. Lakini kumjua Mungu si lengo kuu la maisha. Ujuzi hutokana na imani, na imani ni zawadi kutoka kwa Mungu. Lakini kuwa kikamilifu…

Tafakari ya 350: Uzuri katika Kuabudu

Ulimwengu ni mzuri na unadhihirisha uzuri wa Mungu, lakini mambo ya kiroho, kama vile Ekaristi Takatifu, ni mazuri zaidi sana.  Ili kuuona uzuri wa Mungu, aliyepo katika Ekaristi Takatifu Sana, unahitaji macho ya imani.  Mojawapo ya njia bora zaidi za kuuwezesha mtazamo wako kuutambua uzuri huu kwa uwazi zaidi ni kuabudu.  Ingawa kupokea…

Tafakari 349: Kupoteza Amani ya Moyo Wako

Ni nini chenye uwezo wa kuondoa amani na utulivu wa moyo wako?  Je, ingekuwaje kama ungetukanwa, kudhihakiwa, kuhukumiwa kwa uongo, kufungwa gerezani, kupigwa au hata kuuawa?  Je, lolote kati ya haya lingeondoa amani ya Mungu moyoni mwako?  Ni ikiwa tu utaruhusu hilo.  Ni muhimu ujue na uamini…

Tafakari 348: Mungu Hutimiza Anayoyafunua

Inashangaza kuyatafakari mambo mawili ya hakika kwa pamoja.  Kwanza, tafakari jinsi Mtakatifu Faustina alivyomsikia Yesu akimwambia mara kwa mara kwamba alitaka Sikukuu ya Huruma ya Mungu itangazwe rasmi na kuadhimishwa katika Jumapili ya Pili ya Pasaka kila mwaka.  Je, mtawa huyu wa kike, mnyenyekevu aliyeishi maisha ya kujitenga monasterini, angewezaje kutimiza jukumu kama hilo…

Tafakari 347: Komunyo Takatifu

Hakuna zawadi kubwa zaidi ulimwenguni humu kuliko Komunyo Takatifu.  Hata hivyo, mara nyingi tunaikaribia Sakramenti hiyo tukiwa na mioyo iliyotawanyika na isiyo makini.  Ili kushinda hali hiyo ya kutawanyika, lazima kwanza usadiki, kwa akili yako yote, kweli za kina kuhusu uhalisi wa Komunyo Takatifu.  Lazima ujisalimishe…