Kiswahili

Tafakari ya 124: Huruma ya Sala ya Maombezi

Je, unataka kuona Huruma ya Mungu ikimiminika kwa wingi juu ya ulimwengu?  Tunatumaini na kudhani kwamba jibu la swali hilo ni “Ndiyo” isiyo na kusita.  Ni muhimu kujua kwamba, kwa namna fulani, unawajibika kwa kutokea au kutotokea kwa jambo hilo.  Hasa, Yesu…

Tafakari ya 123: Baraka ya Kudhalilishwa

Ni nani mwenye akili timamu angetaka kudhalilishwa?  Ungefanya nini kama ungedhalilishwa?  Watu wengi wangeshawishika kutafuta njia za kuepuka kudhalilishwa. Wengine wangeumia sana moyoni kutokana na hali hiyo.  Wengine wangekasirika na kuanza kujitetea.  Na ingawa…

Tafakari ya 121: Bustani ya Siri Ndani ya Moyo Wako

Fikiria kwamba nyumba yako ilikuwa na ua wa ndani, uliojificha, ambamo ulikuwa na bustani.  Hakuna aliyejua kuhusu bustani hii ya siri.  Palikuwa mahali ulipopanda, kulima, kufanya kazi kwa bidii, kupalilia na kuvuna.  Kisha mazao ya bustani hii yaligawiwa kwa siri kwa…

Tafakari ya 118: Moyo Mkaidi

Mojawapo ya njia kuu tunazozuia Huruma ya Mungu isiingie katika maisha yetu ni ukaidi.  Hasa, tunaposhikilia kwa ukaidi maoni yetu wenyewe kutokana na kiburi chetu, na hivyo kukataa kuwa wazi kwa ukweli, tunaufunga mlango wa neema.  Hii ni…

Tafakari ya 115: Mapenzi ya Mungu Yatakuhifadhi Salama

Mapenzi ya Mungu ni zaidi sana ya mpango wa siku zijazo ambao Mungu amekuandalia.  Ni zaidi ya matumaini na ndoto Zake kwa ajili yako.  Mapenzi Yake ndiyo njia yako ya kuelekea utakatifu, nayo ni chemchemi ya faraja na furaha kuu.  Mapenzi Yake yana namna ya kutenda na pia ya kutotenda (kuruhusu).  Ni…

Tafakari ya 110: Miale ya Huruma

Huruma ya Moyo wa Yesu inang’aa kwa uangavu mkuu. Hii ndiyo iliyokuwa picha ya Huruma ya Mungu ambayo Mtakatifu Faustina aliiona. Moyo ulio wazi wa Bwana wetu ulifurika, ukimimina mwanga na neema juu ya ulimwengu. Yesu anataka kuendelea kuuangazia ulimwengu…

Tafakari 108: Sauti ya Kanisa

Mungu amesema na watakatifu kwa njia nyingi, ikiwa ni pamoja na kupitia neema nyingi za ndani na misukumo ya kiroho.  Lakini hata mwanafumbo mkuu kuliko wote, aliye katika kilele cha utakatifu, hatimaye lazima aitii Sauti ya Mungu inayosema kupitia Kanisa Lake.  Kanisa, hasa…

Tafakari ya 107: Kuifunua Nafsi Yako katika Ungamo

Mungu anatutumia mapadri Wake kuwa wawakilishi Wake.  Ingawa mapadri si wakamilifu, bado wao ni wawakilishi wa Mungu.  Hili ni kweli hasa katika Sakramenti ya Upatanisho.  Ni muhimu tuikaribie Sakramenti hiyo…

Tafakari ya 106: Kulala katika Kristo

Kila usiku, unapokwenda kulala, unaalikwa kulala katika neema na Huruma ya Bwana wetu.  Unaalikwa kupumzika mikononi Mwake ili upate nguvu mpya na uchangamfu.  Usingizi ni mfano wa sala na, kwa kweli, unaweza kuwa namna ya kusali.  Kupumzika ni kupumzika katika Mungu.  Kila…

Tafakari ya 100: Tamaa ya Kutenda Mema

Mungu hututabasamia na kutujalia thawabu tele kwa upendo tunaomwonyesha Yeye na wengine.  Matendo yetu ya upendo, yanapochochewa na neema Yake, hugeuzwa kuwa hazina Mbinguni.  Lakini si hayo tu yanayogeuzwa kuwa hazina.  Hata tamaa yetu ya kutenda mema…