Kiswahili

Tafakari 40: Kuingia ndani ya Moyo wa Bwana Wetu

Chembe ya vumbi au punje ya mchanga huwa haina umuhimu mkubwa katika hali nyingi.  Hakuna anayetambua chembe moja au punje moja uani au hata sakafuni ndani ya nyumba.  Lakini mojawapo ikiingia jichoni, punje au chembe hiyo hutambulika mara moja.  Kwa nini?  Kwa sababu…

Tafakari ya 33: Huruma ya Utakaso

Hebu fikiria kama ungeweza kuiona roho yako kama Mungu anavyoiona.  Ungeona nini?  Mungu anaionaje roho yako?  Hakika anamwona mtoto Wake wa thamani na anakutazama kwa upendo mkuu kabisa.  Lakini pia anaiona dhambi yako, hata iliyo ndogo kabisa.  Dhambi hizi, hata kasoro ndogo kabisa…

Tafakari ya 32: Huruma ya Kusamehe

Katika maisha yako yote, utaumizwa na dhambi za wengine. Hili haliepukiki. Swali la msingi la kutafakari ni jinsi unavyoyashughulikia maumivu haya. Je, utayang’ang’ania na kuendelea kuyawazia kwa uchungu? Au utasamehe? Lakini kusamehe hakutoshi. Lazima uiruhusu Huruma ya Mungu iingie ndani ya roho yako kiasi kwamba…

Tafakari 342: Burudisho la Mateso ya Kristo

Kwa kawaida hatuyaweki pamoja maneno “mateso” na “burudisho”. Je, Mateso ya Kristo yanawezaje kuburudisha? Kwa mtazamo wa kidunia, ni ya kutisha na ya kuhuzunisha tu. Bwana aliteseka sana, na Mama yetu mbarikiwa aliteseka pamoja Naye akiwa mwenye huzuni kuu…

Tafakari 338: Kutunza Siri

Tendo moja la upendo tunaloweza kumtendea mwingine ni kumtunzia siri.  Sote tumewahi kufikiwa na watu wenye tatizo au waliochanganyikiwa, nao wakatuomba tusimwambie mtu mwingine.  Je, unaweza kuitunza siri takatifu ya namna hii?  Kutunza siri ni tendo zuri sana la huruma kwa wengine.  Ikiwa…

Tafakari 337: Kuwasaidia Wengine Wenye Mahangaiko

Katika maisha yetu, ni karibu hakika kwamba mara kwa mara tutakutana na watu wenye fadhaa, waliofadhaika au wenye wasiwasi. Huenda wakawaza kupita kiasi kuhusu hili au lile, na hata mawazo yao yakakosa mantiki kwa kiasi fulani. Hii ni fursa iliyojaa neema ya kutenda Huruma. Mahangaiko…

Tafakari 335: Kusamehe Daima

Mojawapo ya mambo magumu zaidi kufanya maishani ni kuwaombea wale wanaokutesa na kuwatendea kwa heshima na huruma kubwa kabisa.  Lakini kuna faida gani katika kuwachukia au kuwashambulia kwa hasira?  Kuwatendea “madhara” hayo kunaiharibu nafsi yako mwenyewe zaidi sana kuliko nafsi zao.  Samehe…

Tafakari 334: Kuzihudumia Roho

Mojawapo ya baraka kuu zaidi tulizopewa ni uwezo wa kuwatumikia wengine.  Tunawatumikia kwa njia nyingi, hasa kulingana na wito wa kila mmoja wetu.  Lakini huduma kuu zaidi tunayoweza kumpa mtu ni kuwa mhudumu wa Huruma ya Mungu, tukimwongoza kwenye utukufu…